Posts

Showing posts from September, 2024

NLD YAVUNA WANACHAMA ADC NA ACT WAZALENDO

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  WANACHAMA 150 kutoka ADC na ACT wamejiunga na NLD na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho,  Doyo Hassan Doyo. Wanachama hao, wakiongozwa na Mariam Sijaona aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ACT Wazalendo na Scola Kahana aliyekuwa mgombea wa nafasi ya makamo mwenyekiti bara kupitia ADC na mgombea ubunge jimbo la kibaha katika uchaguzi wa 2020, leo tarehe 29-09-2024 wamejiunga na Chama cha NLD. Doyo, pamoja na viongozi wengine wa NLD, akiwemo Makamo Mwenyekiti Bara,  Khamis Said Hamad, waliwakaribisha wanachama hao wapya na kuwahakikishia kuwa wana haki sawa na wanachama wa chama hicho kwa mujibu wa katiba ya NLD. Wanachama hao wamesema kuwa wameamua kujiunga na Chama cha NLD kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kuunga mkono juhudi za  Doyo katika kukuza demokrasia nchini. "Tunajua chama chetu kipya hakina ruzuku, lakini tupo tayari kukaa na njaa ili kupigania demokrasia ya kweli na hatimaye chama chetu kufanya vizuri...

CARITAS TABORA YATOA VYEREHANI VYA ZAIDI YA M.17 KUSAIDIA WANAWAKE VIJIJINI

Image
Na Benny Kingson,DmNewsOnline TABORA  JUMLA ya vyerehani 54 vyenye thamani ya sh.milioni 17,820,000 vimetolewa na idara ya maendeleo ya jamii ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora CARITAS  kwa wanawake ‘walea pweke’ wa Vijiji vya wilaya ya Uyui Mkoani humo kwa lengo la kuonyesha upendo kwao na kuwakwamua kuichumi. Mkurugenzi wa CARITAS Mkoani Tabora Padri Paschal Kitambi akikabidhi vyerehani hivyo kwa wanawake hao ‘Single mother’ katika Kata ya Isikizya wialayani humo alisema kuwa lengo la msaada huo ni kuonyesha upendo wao  kwa vitendo  na kuwakwamua kimaisha. Padri Kitambi amesema kuwa idara hiyo imewashika mkono akinamama hao ambapo nao wanatakiwa kuinuka na kuendeleza jitihada za kujipatia vipato,kujiimarisha kiuchumi na hatimaye kujiletea maendeleo yao na kuwa mfano bora kwa jamii. ‘CARITAS imewashika mkono na mkumbuke Kanisa linasisitiza upendo kupitia salamu ama kauli mbiu yetu ya dini mbalimbali,upendo na amani,hivyo na nyie msimame msonge mbele na kuonyesha...

MWISHO WA KULIPA KODI YA MAPATO YA AWAMU YA TATU NI LEO TAREHE 30 SEPTEMBA 2024.

Image
MAMLAKA YA MAPATO NCHINI TRA IMETANGAZA KUWA SEPTEMBA 30 NI MWISHO WA KULIPA KODI YA MAPATO

MANALA MBUMBA AENDELEA KUIGUSA JAMII WILAYANI KAHAMA.

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline KAHAMA  MHANDISI  Manala Mbumba,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Manala amewashika mkono kanisa la waadventista wasabato lililopo Kagongwa-Kahama Kwa Kuchangia shilingi laki 1.5 Manala ambaye pia ni mzaliwa wa Mkoa wa Shinyanga Wilayani Kahama amekuwa akijipambanua katika maeneo tofauti tofauti hususani kwenye jamii kupitia Taasisi hiyo ili kusaidia Watanzania . Akizungumza na DmNewsOnline akiwa wilayani Kahama amesema kuwa anarudisha Kwa jamii katika kile kidogo anachokipata kupitia Taasisi yake ya Manala na hiyo inatokana na Yeye kutoka familia ya kipato cha chini hivyo ni vyema kwake kushiriki Katika kuwainua wengine. Manala amesema taasisi hiyo yenye makao makuu Wilayani Kinondoni  jijini Dar es salaam ipo Kwa ajili ya Watanzania wote  Katika hafla hiyo ya Kuchangia kanisa ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kidini ikiongozwa na Mbunge wa kisesa Luhaga Mpina,ambapo alihimiza wananchi kujenga tamaduni ya kus...

VIJANA UVCCM WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUONYESHA MEMA YANAYOFANYWA NA SERIKALI.

Image
Na Eliasa Ally DmNewsOnline   IRINGA  Akizungumza  Leo septamba 19,2024 wakati wa kufunga mafunzo maalum ya vijana wa CCM kutoka kata mbalimbali za Mkoa wa Iringa, yaliyofanyika katika Chuo cha Vijana Ihemi, MNEC Asas alisema ni muhimu vijana kuwajibu wanaomchafua Rais, badala ya kutumia mitandao kujipiga picha zisizo na maana. “Asas alisema, inashangaza kuona Rais anashambuliwa mitandaoni na watu wasiokuwa na nia njema vijana wamenyamaza kimya na kushindwa kuwajibu wenye nia ovu, jambo ambalo linaweza kuonekana kama ukweli.’” Aidha amesema vijana wa UVCCM wako vizuri kwenye hamasa lakini niwaombe sana mtumie vizuri mitandao ya kijamii wenzetu wamekosa sera kutokana na kazi nzuri inayofanywa na serikali yetu wameamua kuanza kumchafua kiongozi wetu mkuu na serikali yetu hili halikubaliki ni lazima wakanushwe kwa kueleza kazi nzuri inayofanywa na mama yetu. Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Aisha Mpuya, alieleza kuwa mafunzo hayo ya siku saba yalikuwa na mada mbalimbali ikiwe...

WANASIASA NCHINI WATAKIWA KUFANYA SIASA ZA KUTUMIA LUGHA ZA STAHA

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  KATIBU Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo amewataka wanasiasa nchini   kufanya siasa za kistaarabu na kutumia lugha za staha na sio siasa za  kudhalilisha na kuchafua watu kwa kutweza utu wao. Kauli hiyo imetolewa  Septemba 29,2024 na Katibu  Mkuu wa NLD Doyo Hassan  katika Uzinduzi wa program ya operesheni ya fyeka CCM  kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 uliofanyika katika ofisi za Makao makuu ya chama hicho zilizopo Tandika Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.  "Juzi Kuna Kongamano la chama fulani la wanawake lilikuwa likimtuhumu Rais kuwa ni muuaji hiyo siyo sawa kwani kama Mungu amekupangia kifo utakufa tuu"amesema Doyo  Amesema kuwa chama hicho kimesikitishwa na tuhuma za chama hicho na kuviomba vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa wanaomchafua Rais  "Chama kitafanya siasa safi na kutoa wito kwa wanachama wake kutotoa maneno y...

WANANCHI KUWENI MABALOZI KATIKA KUZUIA AJALI ZA BARABARANI - NAIBU WAZIRI SILLO

Image
Na Eliasa Ally,DmNewsOnline  IRINGA NAIBU  Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Daniel Sillo amewataka wananchi wote bila kujali jinsia zao  kujitolea na  kuwa mabalozi katika kuzuia ajali za barabarani zinazosababisha vifo, majeruhi na wakati mwingine ulemavu wa kudumu.  Sillo ameyasema hayo Septemba 28, 2024 mkoani Iringa kwenye Maadhimisho ya miaka kumi ya Shirika la Mabalozi wa Usalama barabarani Tanzania toka kuanzishwa kwake ambapo wadau mbalimbali wa usafirishaji na wananchi wamehudhuria. Aidha, akizungumza kwenye hafla hiyo ambayo imehudhuliwa pia na askari kutoka Jeshi la polisi, Zimamoto na uhamiaji, Sillo amesema kuwa, jamii inapaswa kutambua mapambano dhidi ya ajali za barabarani ni jukumu letu sote hivyo tunapaswa kukumbushana, kutoa elimu lakini pia kukemea vitendo vya uvunjaji wa Sheria za usalama barabarani. Ameongeza kuwa, madhara makubwa ya ajali za barabarani huwakumba wanawake na watoto kwani takwimu zinaonyesha kwamba mara nyingi vifo vingi huw...

MATUKIO YA PICHA : KIMBUNGA CHA RAIS SAMIA AKIHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI RUVUMA

Image
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Mkutano wa kuhitimisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Ruvuma tarehe 28 Septemba, 2024.

DIRISHA LA MIKOPO LAFUNGULIWA, TANGA JIJI KUANZA NA BILLION 3

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline TANGA HALMASHAURI  ya Jiji la Tanga imefungua dirisha la utoaji mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani Kwa kina mama, vijana na watu wenye ulemavu, kuanzia leo tarehe 29 Septemba 2024, na litakuwa wazi kwa mwezi mmoja, na kufungwa Oktoba 29 ambapo Serikali imefanya maboresho ya sheria na kanuni za mikopo hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini, amesema Halmashauri imeidhinisha kiasi cha zaidi ya shilingi Billion 3, ambapo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanachagua biashara yenye manufaa na si kuiga biashara ambazo hawana elimu nazo, huku akitoa wito kwa maofisa mikopo kujiepusha na undugu, na kufuata kanuni zilizowekwa na Serikali. Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga Simon Mndende amesema kuwa matarajio yao kwa Halmashauri nikuhakikisha wanakopesha vikundi visivyo pungua 135 ndani ya kata 27 zilizopo Jijini humo. Mndende amesema kwa marekebisho...

RAIS SAMIA AFUNGUA KIKAO MAALAMU CHA UWT

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline RUVUMA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Taifa katika ukumbi wa Parokia ya Bombambili, Wilaya Songea Mkoani Ruvuma, leo tarehe 28 Septemba, 2024.

WADAU WA UTALII WATAKIWA KUUNGANISHA NGUVU YA KULINDA MALIASILI KWA AJLI YA UTALII ENDELEVU

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline ARUSHA WADAU wa Utalii wametakiwa kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kulinda maliasili na tamaduni zilizopo nchini Tanzania ili kuwa na biashara ya utalii endelevu lakini pia wametakiwa  kubuni mbinu mpya za kutangaza na kuendeleza biashara ya utalii nchini. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) wakati wa maadhimisho ya siku ya Utalii Duniani Jijini Arusha ambayo yameandaliwa na  shirika lisilo la kiserikali la Rethinking Tourism Africa kwa kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Kitandula katika hotuba yake alipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii kupitia filamu za Tanzania The Royal Tour na Amazing Tanzania kwa kuwa zimekuwa kichecheo kikubwa kwa wageni kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini. Kupitia filamu ya Tanzania The Royal Tour, imepelekea idadi ya watalii kuongeza kufikia milioni moja na laki nane kwa takwimu za Januari...