MANALA MBUMBA AENDELEA KUIGUSA JAMII WILAYANI KAHAMA.



Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
KAHAMA 

MHANDISI  Manala Mbumba,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Manala amewashika mkono kanisa la waadventista wasabato lililopo Kagongwa-Kahama Kwa Kuchangia shilingi laki 1.5

Manala ambaye pia ni mzaliwa wa Mkoa wa Shinyanga Wilayani Kahama amekuwa akijipambanua katika maeneo tofauti tofauti hususani kwenye jamii kupitia Taasisi hiyo ili kusaidia Watanzania .

Akizungumza na DmNewsOnline akiwa wilayani Kahama amesema kuwa anarudisha Kwa jamii katika kile kidogo anachokipata kupitia Taasisi yake ya Manala na hiyo inatokana na Yeye kutoka familia ya kipato cha chini hivyo ni vyema kwake kushiriki Katika kuwainua wengine.

Manala amesema taasisi hiyo yenye makao makuu Wilayani Kinondoni  jijini Dar es salaam ipo Kwa ajili ya Watanzania wote 

Katika hafla hiyo ya Kuchangia kanisa ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kidini ikiongozwa na Mbunge wa kisesa Luhaga Mpina,ambapo alihimiza wananchi kujenga tamaduni ya kushiriki katika kusaidia jamii na Kuchangia maendeleo endelevu Kwa kupitia taasisi  za kidini.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025