VIJANA UVCCM WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUONYESHA MEMA YANAYOFANYWA NA SERIKALI.
Na Eliasa Ally DmNewsOnline
IRINGA
Akizungumza Leo septamba 19,2024 wakati wa kufunga mafunzo maalum ya vijana wa CCM kutoka kata mbalimbali za Mkoa wa Iringa, yaliyofanyika katika Chuo cha Vijana Ihemi, MNEC Asas alisema ni muhimu vijana kuwajibu wanaomchafua Rais, badala ya kutumia mitandao kujipiga picha zisizo na maana.
“Asas alisema, inashangaza kuona Rais anashambuliwa mitandaoni na watu wasiokuwa na nia njema vijana wamenyamaza kimya na kushindwa kuwajibu wenye nia ovu, jambo ambalo linaweza kuonekana kama ukweli.’”
Aidha amesema vijana wa UVCCM wako vizuri kwenye hamasa lakini niwaombe sana mtumie vizuri mitandao ya kijamii wenzetu wamekosa sera kutokana na kazi nzuri inayofanywa na serikali yetu wameamua kuanza kumchafua kiongozi wetu mkuu na serikali yetu hili halikubaliki ni lazima wakanushwe kwa kueleza kazi nzuri inayofanywa na mama yetu.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Aisha Mpuya, alieleza kuwa mafunzo hayo ya siku saba yalikuwa na mada mbalimbali ikiwemo kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa, kuelewa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita lakini pia kujifunza matumizi bora ya mitandao.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Agrey Tonga, alimhakikishia MNEC Asas kwamba jumuiya hiyo ipo imara na itazingatia ushauri wake na kutekeleza mafunzo waliyojifunza ili kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola kama alivyosema
Comments
Post a Comment