DIRISHA LA MIKOPO LAFUNGULIWA, TANGA JIJI KUANZA NA BILLION 3



Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
TANGA

HALMASHAURI  ya Jiji la Tanga imefungua dirisha la utoaji mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani Kwa kina mama, vijana na watu wenye ulemavu, kuanzia leo tarehe 29 Septemba 2024, na litakuwa wazi kwa mwezi mmoja, na kufungwa Oktoba 29 ambapo Serikali imefanya maboresho ya sheria na kanuni za mikopo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini, amesema Halmashauri imeidhinisha kiasi cha zaidi
ya shilingi Billion 3, ambapo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanachagua biashara yenye manufaa na si kuiga biashara ambazo hawana elimu nazo, huku akitoa wito kwa maofisa mikopo kujiepusha na undugu, na kufuata kanuni zilizowekwa na Serikali.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga Simon Mndende amesema kuwa matarajio yao kwa Halmashauri nikuhakikisha wanakopesha vikundi visivyo
pungua 135 ndani ya kata 27 zilizopo Jijini humo.

Mndende amesema kwa marekebisho ya sheria yaliofanyika kikundi ndio dhamana ya mkopo, japo kila mwanakikundi ana uhuru wa kufanya biashara tofauti ndani ya kikundi.

Aprili, 2023 serikali ilisitisha utoaji wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani nchi nzima
kutokana na changamoto mbalimbali kama vile vikundi kutorejesha mikopo kwa wakati. 

Baada ya hapo serikali iliunda timu ya kuandaa maboresho ya utoaji na usimamizi wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mapendekezo yaliyotolewa na timu iliyoundwa yamepelekea kuandaliwa Kanuni mpya za utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za mwaka 2024.

 Pamoja na mambo mengine, kanuni mpya zimeongeza sifa ya umri wa vijana kutoka miaka 18 - 35 ya awali na kuwa miaka 18 - 45.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025