Posts

Showing posts from June, 2024

CHAMA ATUA JANGWANI ( YANGA SC. )

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kumsajali kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Clatous Chota Chama ambaye ameondoka Simba SC baada ya mkataba wake kumalizika.

TLP YAJITAFUTA,YAPATA MRITHI WA MREMA ,AHAIDI MAKUBWA

Image
Na Richard Murusha,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wamemchagua Injinia Aivan Maganza kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho. Msimamizi wa uchaguzi huo, Rashid Amir, amemtangaza Maganza kuwa mshindi baada ya kupata kura 33. Akizungumza baada ya kuchaguliwa Leo Juni 29,2024  Maganza ameahidi kukibadilisha chama hicho na kuwa cha kisasa huku akituma salamu kwa vyama vingine kwamba vijipange. "Wale ambao wako TLP kwa nia ya kukivuruga chama au kukikwamisha kuanzia sasa nawatangazia waondoke...nataka nibaki na watu wanaoweza kufanya kazi," amesema Maganza. Maganza pia amemteua Riziki Gaga kuwa Katibu Mkuu na kuahidi kuunda upya sekretarieti ya chama hicho. Awali Maganza alikuwa Mwenyekiti wa Vijana TLP. Na kwa upande wake katibu Mwenezi wa chama hicho Geofray Stephen Laizar amesema ni wakati wa kushikamana kwa pamoja pasipo kuangalia dini wala kabila la mtu  Amesema  baada ya kumpata mwenyekiti mpya  chama kit...

KATIBU CCM PWANI ASHUSHA NONDO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Image
Na VictorMasangu,DmNewsOnline PWANI  CHAMA  cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kimejiwekea mipango kabambe  ya kuhakikisha  kwamba wanapata wagombea wazuri  na wenye sifa ambao wanakubalika katika jamii  na kuweza kusabisha kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo. Hayo yamebainishwa na Katibu wa (CCM)  Mkoa wa Pwani Bernad Ghathy  wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya (CCM) Mkoa ambapo amesema kuwa lengo kubwa la chama ni kuweka misingi imara ya kuwapata viongozi wazuri ambao watakwenda kuipeperusha vyema bendera ya chama kwa kushinda katika mitaa yote ndani ya Mkoa wa Pwani. Katibu Ghaty amesema kwamba kikao hicho cha Halmashauri kuu kimeelekeza kwamba katika vikao vyote vya  uteuezi  vitakavyofanyika katika ngazi ya chama  vihakikishe kwamba vinatenda haki bila upendeleo wowote  katika kuwapata viongozi ambao watagombea katika uchaguzi huo wa serikali z...

RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI AZINDUA BOHARI YA KUHIFADHI NISHATI YA GESI YA ORYX ZANZIBAR

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  ZANZIBAR    KAMPUNI ya Oryx Gas imeungana na kampuni ya TP Limited yenye makao yake Zanzibar ambayo ni  kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies (Vigor Group), kujenga bohari ya kwanza ya kuhifadhi nishati za gesi ili kuongeza usambazaji wa gesi ya LPG kisiwani humo. Akizungumza  mbele ya wananchi wa Zanzibar baada ya kuzindua bohari hiyo ya kupokea na kuhifadhi gesi na miundombinu mingine jumuishi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amepongeza ujenzi wa bohari hiyo huku akizipongeza taasisi nyingine ambazo zimefanikisha ujenzi wa mindombinu jumuishi ya bandari ya Mangapwani ambayo itahusika na meli za mafuta na gesi pamoja na shughuli nyingine “Kwa muda mrefu tulikuwa tunatumia bandari ya Malindi lakini kutokana na ongezeko la shughuli za kiuchumi bandari ile haitoshi, hivyo Serikali ilitangaza eneo la Mangapwani kuwa bandari kwa ajili ya nishati ya gesi, mafuta na miundombinu me...

MISA-TAN YAOMBA KUPUNGUZWA KWA ADA YA LESENI ZA MITANDAO YA KIJAMII.

Image
Mwandishi Wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM                TAASISI ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN), imeiomba serikali kupunguza viwango vya ada ya kuendesha mitandao ya kijamii (Blogs, Online Tv na YouTube ili kuvutia vijana kumiliki mitandao kisheria na kujiajiri. Aidha MISA-TAN imeomba serikali kuharakisha kuunda baraza huru la habari na mfuko wa kusaidia wanahabari nchini kujiendeleza kielimu. Ombi hilo limetolewa  Juni 26 ,2024 na Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, Mussa Juma  jijini Dar es Salaam, wakati akifunga warsha ya siku moja kwa wanachama zaidi ya 33 wa taasisi hiyo na waandishi wengine kutoka katika vyombo vya habari. Warsha hiyo iliandaliwa na MISA-Tan kwa ushirikiano na Shirika la Protection International Afrika na kudhamiwa na  Serikali ya Finland. Juma amesema, gharama ya sh 500,000 ya leseni ua kumiliki blogs na millioni moja kumiliki luninga za mtandaoni ni kubwa kwa vijana na watu wenye ulemavu. "...

DC KIBAHA AMSHUKURU RAIS. DKT SAMIA,MBUNGE KOKA , UJENZI WA DARAJA JIPYA MTO MPIJI

Image
Na Victor Masangu,DmNewsOnline  KIBAHA   Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amempongeza Rais kwa kuweza kutoa fedha  kiasi cha shilingi bilioni 4  kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa  daraja jipya la kudumu katika  mto mpiji ambalo litaweza kuwa mkombozi kwa wananchi kuvuka bila shida hasa katika kipindi cha mvua. Darala hilo la mto mpiji ambalo kwa sasa limejengwa kwa muda  limekuwa ni kiunganishi na mkombozi mkubwa  kwa wananchi kutoka   Wilaya mbili za Kibaha Mkoa wa Pwani pamoja na Wiyaya ya Ubungo ya Jijini Dar es Salaam Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi hizo Leo Juni 26,2024  wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa daraja la muda kutoka kwa kaimu mkuu wa mafunzo na operesheni wa Jeshi la la nchi kavu Brigadia Jenerali Stanley Mjelwa halfa ambayo imehudhuliwa na viongozi wa serikali,chama,wananchi na Tarura. Nikson amebainisha  kwamba pia   amemshukuru kwa dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvest...

DC ATAKA KUANZISHWA MIRADI YA KIELELEZO KALIUA

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline TABORA  HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora imepongezwa kwa kuweka rekodi ya kufanya vizuri katika utekelezaji shughuli za maendeleo ya wanachi ikiwemo kuendelea kupata hati safi kila mwaka kwa kuweka vizuri taarifa zake. Hayo yamebainishwa Leo  Juni 26 ,2024 na Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Rashid Chuachua alipokuwa akizungumza na Madiwani, Wataalamu na Watendaji wote wa halmashauri hiyo katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani. Amesema kuwa halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri chache nchini zinazofanya vizuri sana katika suala zima la utekelezaji shughuli za maendeleo kupitia fedha zake za ndani na zile za serikali kuu ikiwemo kuingiza mapato mengi Amesisitiza kuwa hayo yote yanachochewa kwa kiasi kikubwa na kazi nzuri yenye weledi na mshikamano mzuri wa Waheshimiwa madiwani, Wataalamu, Watendaji wa Vijiji na Kata na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Jerry Mwaga. ‘Halmashauri Kaliua inafanya kazi nzuri sana, na kila mwaka...

JOTO LA UCHAGUZI WA MWENYEKITI CCM TABORA LAPANDA

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline TABORA WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora wanasubiri kwa hamu kubwa kupata Mwenyekiti mpya wa Chama hicho atakayewaongoza kwenye kinyanga’anyiro cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwakani.   Akizungumza na DmNewsOnline Leo Juni 26,2024  Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa, Idd Moshi amesema kuwa mchakato wa kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wao Mzee Hassan Mohamed Wakasuvi aliyefariki ghafla Februari 21 mwaka huu upo katika hatua za mwisho. Amesema kuwa kwa sasa wanachosubiri ni uteuzi wa mwisho wa majina ya wagombea watakaoingia kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ridhaa ya wanaCCM wa Tabora kupitia kura zao. ‘Muda wowote Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitaketi na kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi hiyo, baada ya zoezi hilo kukamilika na kuletewa majina tutawatangazia wana Tabora tarehe ya uchaguzi’, amesem Komredi Idd amebaini...

RC CHACHA APONGEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO KALIUA

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline  TABORA OFISI ya Mkurugenzi, Madiwani, Wataalamu na Watendaji wa halmashauri  ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora wamepongezwa kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na kasi nzuri ya ukusanyaji mapato kutoka katika vyanzo vyake. Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Matiko Chacha alipokuwa akizungumza na watendaji hao katika kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo cha mapitio ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG). Amesema kuwa halmashauri zote 8 za Mkoa huo zinafanya vizuri lakini halmashauri Kaliua ina kasi kubwa zaidi kwani mwishoni mwa mwezi Mei 2024 walikuwa wamekusanya sh bil 6.5 ambazo ni zaidi ya asilimia 100 ya malengo yao. RC  Chacha amebainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mkoa huo ulikisia kukusanya jumla ya sh bil 39 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani lakini kabla ya mwaka wa fedha kumalizika kiasi cha sh bil 33.4 zilikuwa zimekusanywa. ‘Nawapongeza kwa mshikamano mzuri w...

KANISA LATOA MSAADA WA CHAKULA KWA KAYA ZAIDI YA 100

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline TABORA KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) Maranatha Miracle Centre lililopo eneo la Cheyo katika Halmashauri ya Manispaa Tabora limetoa msaada wa chakula kwa kaya zaidi ya 100 zenye uhitaji mkubwa ili kuwawezesha kuishi. Akizungumza na DmNewsOnline Leo Juni 26 ,2024  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Rev.Lutengano Mwasongela amesema kuwa wametoa msaada huo kama sehemu ya mchango wa kanisa hilo kwa jamii inayowazunguka ili kudumisha mahusiano mazuri. Ameongeza kuwa wametoa mchango huo ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya 6 inayaoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha jamii ya Watanzania haifi na njaa. Rev.Mwasongela amebainisha kuwa kanisa lake limekuwa likitoa msaada huo kwa nyakati tofauti ikiwemo kipindi cha sikukuu za pasaka na krismas kwa lengo la kurejesha furaha katika mioyo ya waliokata tamaa. Amefafanua kuwa katika wiki kanisa la TAG Maranatha Miracle Centre limeendeleza utaratibu huo kwa kufanya matendo me...

EMIRATES SKYWARDS EXPANDS ITS BRAND PORTFOLIO, ATTRACTING 33 MILLION MEMBERS WORLDWIDE

Image
DmNewsOnline,Dar Es Salaam Emirates Skywards, the award-winning loyalty program of Emirates, continues to revolutionize the loyalty industry with its innovative initiatives and customer-focused strategy.  Over the past year, the program has introduced exciting new features and expanded its brand portfolio, attracting 33 million members worldwide. Here are five ways Emirates Skywards has enhanced the loyalty experience for its Tanzanian members:- - Exclusive Skywards Experiences ., Members can now enjoy unique opportunities through Skywards Exclusives, such as hospitality tickets and VIP experiences at major sporting events like the US Open and Wimbledon. Additionally, new lifestyle partnerships offer experiences like visiting Sri Lanka's tea plantations with Dilmah Tea and exploring France's vineyards -Cash+Miles Flexibility. , The popular Cash+Miles feature has been expanded, allowing members to reduce the cash needed for flights, ancillary products like seat selection, excess...

WIZARA TATU KUJADILI ,TALAKA, VIFO.

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline DODOMA WAZIRI wa Katiba na Sheria Balozi Dk Pindi Chana amesema amepanga kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kutafuta suluhisho la ongezeko la vifo na wimbi la talaka katika jamii. Kwa mujibu wa taarifa ya takwimu ya matukio muhimu ya binadamu ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), takwimu inaonesha kumekuwa na ongezeko la vifo kwa wanaume vinavyosababishwa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza jambo ambalo linasababisha ongezeko la watoto waishio kwenye mazingira yasiyo bora kutokana na kukosa malezi ya pande zote mbili. Aidha Waziri Chana amesema kwa upande wa hali ya ndoa, takwimu inaonesha ongezeko la usajili wa talaka limekuwa kubwa kwa kila mwaka jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa ukatili kwa watoto kwa kukosa malezi ya wazazi wawili. Akizindua taarifa ya takwimu ya matukio muhimu ya binadamu pamoja na kufungua mafunzo ya ue...

RUNGU LA DC SAME KUWASHUKIA WAZAZI WANAOTUMIA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO KAMA MTAJI KULIPANA FEDHA.

Image
Ashrack Miraji ,DmNewsOnline  SAME KIKIMANJARO MKUU  wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewaonya baadhi ya wazazi wanaotumia kesi za ukatili wa kijinsia kwa watoto kama mtaji kulipana fedha pindi anapofanyiwa ukatili kuacha mara moja tabia hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuathiri saikolojia na afya ya mtoto pamoja na kumfanya ashindwe kutimiza ndoto zake. Amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi uliofanyika Kata ya Mamba Myamba, ambapo amewasisitiza wananchi hao kutowaficha watuhumiwa wa vitendo hivyo kwenye jamii ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki. “Niwaombe sana wazazi muwalinde watoto wenu, jengeni urafiki na watoto wenu ili waweze kuwaambia madhara ambayo wanayapata huko njiani wanapoenda shule na kurudi watawaambia, na bahati mbaya sisi wazazi hatuwafuatilii watoto tupo bize na kilimo cha tangawizi hatuna muda wa kukaa na watoto wetu watoto wetu wameingia kwenye hivyo vitendo wakati mwingine sio...

GODFREY MZAVA : RAIS SAMIA AMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI NCHINI.

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline  IRINGA  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mzava amesema  Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ili waweze kuweleza.  Mzava ameyasema hayo Leo Juni 25, 2024  mkoani Iringa wakati akizindua kituo cha Mafuta cha Asas kilichopo eneo la kituo kikuu cha mabasi mkoani humo wenye thamani ya Bilioni 1.  Mzava dhamira ya Rais Samia ni kuhakikisha anasogeza karibu sekta binafsi ili ziweze kufanya kazi na kuleta tija kwa Taifa. Amesema ili kufikia adhma hiyo Mhe. Rais amezielekeza  taasisi zote za kibiashara na uwekezaji  kuhakikisha  zinaandaa mazingira rafiki, wezeshi na rafiki pasipokuwa na rasimu ili kuwavutia wawelezaji. "Ninapongeza kampuni ya Asas kwa kuweleza kituo cha Mafuta kama walivyosema kwenye risala yao kuwa kitaendelea kutoa huduma kwa wananchi hasa watumiaji wa kituo  ...

HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAPATA HATI SAFI

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  KIBAHA MKUU wa Mkoa Pwani Abubakar Kunenge ameipongeza Halmashauri ya Mji Kibaha kwa kupata hati safi kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha kilichofanyika Kibaha wakati wa kupitia hoja za CAG. Kunenge amesema kuwa Halmashauri imefanya vema kwa ukusanyaji wa mapato kutoka asilimia 54 Februari na kufikia asilimia zaidi 100 ambapo ni kazi kubwa imefanyika. "Nawapongeza kwa kazi kubwa mliyoifanya lakini mnapaswa kudhibiti matumizi ya fedha kwani baadhi ya hoja zimetokana matumizi ya fedha na kutekeleza miradi kwa wakati,"amesema Kunenge. Kwa upande wake katibu wa baraza hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dk Rogers Shemwelekwa amesema kuwa kulikuwa na jumla ya hoja 69 zikiwemo za nyuma ambapo hoja 31 zimefungwa. Shemwelekwa alisema kuwa hoja 38 ambazo hazijatekelezwa ni kutokana na masuala ya kisera lakini wanaendelea kuzifanyia kazi ili z...

NCAA YAZITAKA BAADHI YA TAASISI KUACHA UPOTOSHAJI KUHUSU WANANCHI WANAOHAMA KWA HIARI NGORONGORO.

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline  NGORONGORO MAMLAKA  ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezitaka baadhi ya taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka ndani na nje ya nchi kuacha upotoshaji kuhusiana na zoezi la kuhamisha wananchi kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wanaojiandikisha kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera na badala yake kutafuta ukweli kuhusu suala hilo. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa tamasha la jamii ya wamasai lililofanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma wa mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema baadhi ya taasisi zimekuwa zikiripoti kwamba kabila la wamasai wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo wamekuwa wakifukuzwa na kuondolewa kwa nguvu. Amesema habari hizo si cha kweli na ndio maana hata tamasha hilo lililofanyika ndani ya kreta ya Ngorongoro kuhudhuriwa  na watu mbalimbali wakiwemo watumishi na  NCAA ilitoa kibali. Amesema jamii ya kimasai, wahadzabe, wamang’ati wanaoishi ndani ya hifadhi imekuwa na us...