RUNGU LA DC SAME KUWASHUKIA WAZAZI WANAOTUMIA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO KAMA MTAJI KULIPANA FEDHA.




Ashrack Miraji ,DmNewsOnline 
SAME KIKIMANJARO


MKUU  wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewaonya baadhi ya wazazi wanaotumia kesi za ukatili wa kijinsia kwa watoto kama mtaji kulipana fedha pindi anapofanyiwa ukatili kuacha mara moja tabia hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuathiri saikolojia na afya ya mtoto pamoja na kumfanya ashindwe kutimiza ndoto zake.

Amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi uliofanyika Kata ya Mamba Myamba, ambapo amewasisitiza wananchi hao kutowaficha watuhumiwa wa vitendo hivyo kwenye jamii ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

“Niwaombe sana wazazi muwalinde watoto wenu, jengeni urafiki na watoto wenu ili waweze kuwaambia madhara ambayo wanayapata huko njiani wanapoenda shule na kurudi watawaambia, na bahati mbaya sisi wazazi hatuwafuatilii watoto tupo bize na kilimo cha tangawizi hatuna muda wa kukaa na watoto wetu watoto wetu wameingia kwenye hivyo vitendo wakati mwingine sio kwamba wanapenda wanatishwa na hao mabazazi”. Amesema DC Kasilda….

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Polisi Kitengo cha dawati la jinsia Wilaya ya Same Tarafa ya Mamba Myamba inashika nafasi ya pili kati ya Tarafa sita za Wilaya hiyo kuripotiwa kwa kesi za ukatili wa kijinsia ikiwemo mapenzi ya jinsia moja (Ushoga), baadhi wa wanajamii kuficha watuhumiwa wa vitendo hivyo miongoni mwa changamoto inayochagiza kuendelea kuwepo kwa matukio hayo.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025