TLP YAJITAFUTA,YAPATA MRITHI WA MREMA ,AHAIDI MAKUBWA
Na Richard Murusha,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wamemchagua Injinia Aivan Maganza kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Rashid Amir, amemtangaza Maganza kuwa mshindi baada ya kupata kura 33.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa Leo Juni 29,2024 Maganza ameahidi kukibadilisha chama hicho na kuwa cha kisasa huku akituma salamu kwa vyama vingine kwamba vijipange.
"Wale ambao wako TLP kwa nia ya kukivuruga chama au kukikwamisha kuanzia sasa nawatangazia waondoke...nataka nibaki na watu wanaoweza kufanya kazi," amesema Maganza.
Maganza pia amemteua Riziki Gaga kuwa Katibu Mkuu na kuahidi kuunda upya sekretarieti ya chama hicho.
Awali Maganza alikuwa Mwenyekiti wa Vijana TLP.
Na kwa upande wake katibu Mwenezi wa chama hicho Geofray Stephen Laizar amesema ni wakati wa kushikamana kwa pamoja pasipo kuangalia dini wala kabila la mtu
Amesema baada ya kumpata mwenyekiti mpya chama kitaunda safu ya ushindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kisha kumsimamisha mgombea kwenye nafasi urais hapo mwakani
Comments
Post a Comment