GODFREY MZAVA : RAIS SAMIA AMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI NCHINI.
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline
IRINGA
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mzava amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ili waweze kuweleza.
Mzava ameyasema hayo Leo Juni 25, 2024 mkoani Iringa wakati akizindua kituo cha Mafuta cha Asas kilichopo eneo la kituo kikuu cha mabasi mkoani humo wenye thamani ya Bilioni 1.
Mzava dhamira ya Rais Samia ni kuhakikisha anasogeza karibu sekta binafsi ili ziweze kufanya kazi na kuleta tija kwa Taifa.
Amesema ili kufikia adhma hiyo Mhe. Rais amezielekeza taasisi zote za kibiashara na uwekezaji kuhakikisha zinaandaa mazingira rafiki, wezeshi na rafiki pasipokuwa na rasimu ili kuwavutia wawelezaji.
"Ninapongeza kampuni ya Asas kwa kuweleza kituo cha Mafuta kama walivyosema kwenye risala yao kuwa kitaendelea kutoa huduma kwa wananchi hasa watumiaji wa kituo kikuu cha mabasi cha mkoa wa Iringa lakini pia kitaongeza mapato ya Halmashauri.
Comments
Post a Comment