Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kumsajali kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Clatous Chota Chama ambaye ameondoka Simba SC baada ya mkataba wake kumalizika.
Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM UONGOZI wa Shirikisho la Vyama vya Waganga wa Tiba Asili Tanzania (Shivyatiata) uliokasimishwa madaraka ya muda wa mwaka mmoja kuliongoza hadi likae sawa, unalalamikiwa na wachama wa vyama vya waganga wa tiba asili nchini kwa kuhodhi madaraka kwa miaka nane kinyume cha sheria na utaratibu waliokubaliana. Wakizungumza na Mwandishi wa DMNews online Tanzania Disemba 31, 2025 baadhi ya wanachama wa vyama vya waganga wa tiba asili kutoka vyama 28 vinavyounda shirikisho hilo, kwamba uongozi uliopo si halali wakidai haukuchaguliwa kikatiba. Pia, wamesema kuwa uongozi huo wa Shirikisho umeshindwa kutimiza majukumu na malengo ya Serikali kuukasimisha madaraka ya muda badala yake unalitumia kujinufaisha wenyewe ikiwamo kufifisha shirikisho kwa kulikosesha dira. Mwenyekiti wa Umoja wa Watengeneza Bidhaa Asili Tanzania (UWABIATA) Rajab Ha...
Na Angelina Mganga -DmNewsOnline BDAR ES SALAAM UCHAGUZI wa nafasi ya Uwenyekiti na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam umefanyika Leo Juni 20,2026,na umemalizika kwa amani na utulivu. Uchaguzi huo ulikuwa na wagombea watatu ambao wamewania nafasi hiyo ya Uwenyeviti wa Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa Mkoa wa Dar es Salaam Wagombe wa nafasi ya Uwenyeviti ni Consolatha M.Rwiza Juma A.Mwingano na Razalous A.Mwakiposa Katika uchaguzi huo Razalous A.Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi hiyo ya Uwenyekiti huku Peppino Sudi Peppino akishinda nafasi ya Katibu. Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo,Msimamizi wa Uchaguzi Kambi Sinde amesema kuwa kura zilizopigwa ni 37 na wagombea walikuwa Consolatha M.Rwiza (11),Juma A.Mwingano (2 )na Razalous A.Mwakiposa ( 24 ) hakuna kura iliyoharibika. Razalous A.Mwakiposa ameshinda Kwa kura 24 kati ya kura 37zilizopig...
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline KOROGWE_TANGA NI Katibu Mkuu (Mstaafu) Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Katibu Mkuu (Mstaafu) Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi Mkuu (DG), na Kamishna wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), sio mwingine bali ni Dkt. Allan Kijazi. Ameonesha nia ya kuendelea kuwatumikia wananchi kupitia Mhimili mwingine wa Bunge baada ya kumaliza kazi, tena iliyotukuka kwenye Mhimili wa Serikali. Ametangaza nia kutaka kuwa Mtumishi wa Wananchi kama Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga. Ana uwezo, ni msikivu, mchapa kazi na mwenye maono. Anafahamu maendeleo makubwa yaliyofanywa na Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo huduma za jamii (Elimu, Afya na Maji). Lakini pia shughuli za maendeleo kwa mtu mmoja mmoja, vikundi na Taifa. Hivyo, yeye anataka kuendeleza pale ambapo watangulizi wake wamefikia il...
Comments
Post a Comment