MAKONDA RC MPYA ARUSHA
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFA32xqRGxZgutwo6nOuCU_ZgFVgFPlOd8Nw3jr3cVZ_-PdpKytMHPHclEV8_0GaES351yVEwjfNAoUIh5p7AfElWMfx5_Az-9S1n_QcodYrK7_phUNtimM4k1CpuM_6LVKEXnQV1sFJk/s1600/IMG_ORG_1711875808799.jpeg)
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline ALIYEKUWA Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Paul Makonda ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha . Makonda anachukua nafasi ya John Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu. Paul Makonda aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kutimkia kwenye ubunge katika Jimbo la kigamboni katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2020. Baada ya kushindwa uchaguzi huo na aliyakuwa Mbunge wa Jimbo hilo Faustine Ndugulile kufanikiwa kutetea Jimbo hilo ,makonda alikuwa nje ya Serikali Kwa muda mrefu kabla ya mapema mwaka huu kuteuliwa na Chama chake kuwa Katibu wa Nec Itikadi ,Uenezi na Mafunzo na Sasa ni mkuu wa mkoa mpya wa Arusha.