UWT WAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO,WAKIWEMO WAFANYABIASHARA KUTOKA CHINA.




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 

KATIBU mkuu wa Umoja  Wanawake Tanzania (UWT)  Jokate Mwegelo amesema kuwa katika kumuunga mkono Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan, umoja huo umejipanga kwa uwekezaji katika sekta ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kumtua mama  kuni kichwani.


Amesema katika kufanikisha hatua hiyo,  Leo Machi 28 ,2024 katika ofisi ndago za Makao makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaamwameweza kukutana  na wadau wa maendeleo kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) pamoja na wafanyabiashara ambapo wamejadiliana mambo mbalimbali..

 Ameongeza kuwa katika nazungumzia yao wameweza kuzungumza mambo mengi mbalimbali lakini Moja ya mambo ambayo wamezungumza na wao wapo tayari kushirikiana nao ni uwekezaji wa upande wa Nishati mbadala itakayoweza kumtua mwanamke mzigo wa Kuni kichwani kwae.


 Jokate amesema wawekezaji hao ambao ujio wao umeratibiwa na Kampuni Canopus Energy Solution, wameonyesha utayari wa kushirikiana katika eneo hilo pamoja na maeneo mengine ya kimkakati.

“Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wetu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kimetoa maelekezo Kwa  jumuiya zote ndani ya  Chama kutazama na kujiendeleza kupitia fursa mbalimbali, hivyo hii kwetu ni fursa tumejipanga kuzalisha nishati mbadala kupitia makaa ya  mawe.

Nakuongeza kuwa "Nikweli Hawa wenzetu hawa kutoka china  wameonyesha utayari na Leo tumefanya mazungumzo ya awali na wametualika kwenda China katika maeneo yao ya uzalishaji na huduma na bidhaa mbalimbali Kwa lengo la  kujionea namna walivyo tayari kutokana na maendeleo ya teknolojia,” amesema.

 Amesema  kuwa UWT ina dhamana kubwa ya kuwaendeleza wanawake wakitanzania hapa nchini kupitia fursa mbalimbali, hivyo imejipanga kuunga mkono juhudi za kumtua mama kuni kichwani kwa kutengeneza Nishati mbadala ambao ni salama kwa afya za binadamu.

Kwa mujibu wa Jokate  Amesema mbali na nishati mbadala, pia wanatazama uwezekano wa kushirikiana na wadau hao katika sekta ya madini na uwekezaji ambapo hilo litafanyika baada ya hatua mbalimbali kutekelezwa na kufanyika Kwa vikao vya ndani  ili kuwa na ushirikiano wenye tija.

Jokate amesisitiza kwamba UWT imejipanga kuchangamkia fursa ambazo zitawanufaisha wanawake katika sekta mbalimbali na kuweza Kukuza viwango vya uchumi wao.

“Fursa yoyote tunayoitengeneza lengo letu ni kuona wanufaika wa kwanza wanakuwa wanawake wa Tanzania,” alisema.

Kwa upande wake Mhandisi Anna Nyangasi kutoka Kampuni ya Canopus Energy Solution, amesema ujio wa ujumbe huo ni fursa kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali hapa nchini 

 Amesema wawekezaji hao wameongezana na Shen Don kutoka Jimbo la Shangzhou ambapo licha ya kukutana na kiongozi huyo mkubwa kutoka umoja wa wanawake Tanzania UWT  pia waliweza kukutana  na wadau mbalimbali.





Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025