BITEKO AMWAGIZA KATIBU MKUU KUMTENGUA MENEJA KAMPUNI
Na Benny Kingson,DmNewsonline
TABORA.
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko amemwagiza Katibu Mkuu wizara ya Nishati kumtengua Meneja Mkuu wa kampuni ya ujenzi wa miundombinu,usafirishaji na usambazi wa shirika la umeme nchini ETDCO Mhandisi Mohamed Abdallah kwa kushindwa kusimamia vema majukumu yake.
Dkt.Biteko ametoa agizo hilo Leo Machi 27 ,2024 wakati akikagua kituo cha kupokea,kupoozea na kusambazia umeme kilichopo Mtaa wa Uhuru,Kata ya Vumilia wilaya ya Urambo Mkoani Tabora .
Dkt.Biteko amesema Meneja huyo ameshindwa kuhudhuria hafla hiyo na kumtuma mwakilishi huku akitambua kuwa amefanya uzembe katika utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho.
Amesema kuwa kampuni hiyo inayoongozwa na Meneja huyo imepeleka nguzo za umeme katika mradi wa ujenzi wa kituo hicho kwa kufikisha asilimia 10 tu hadi sasa ambapo umefikisha aslimia 84 ya utekelezaji mradi huo na kwamba ameonyesha dharau na kufanyakazi kwa mazoea.
“Amemtuma mwakilishi huyo Dismas Masawe,je ni saizi yangu huyu,Katibu Mkuu ebu tafuteni Meneja mwingine,huyo hapana hafai,na sitotaka mazoea na mtu ama kampuni yoyote na lazima tuheshimiane katika kazi,kuna madhaifu makubwa mengi tu nimeyasikia,uswahili mwingi na wizi ndani yake”amesema
Naibu waziri Mkuu huyo amesema Mbunge wa jimbo la Urambo Magreth Sitta amekuwa akipambana kuhakikisha sekta ya umeme, na kilimo zinapata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na ndiyo maana serikali inatekeleza ujenzi wa kituo hicho ili kumaliaza kero zilizokuwa zinawakabili wananchi.
Amesema ujenzi wa kituo hicho wenye kugharimu jumla ya sh.bilioni 40 ukiwa ni umbali wa Km. 115 kutoka mjini Tabora utawezesha maeneo mengine kupata huduma ya umeme na kwamba vituo vingine vimejengwa wilayani Sikonge eneo la Ipole kimejengwa na kufikia asilimia 89,Mlele aslimia 87 na Mpanda Mkoani Katavi umefikia asilima 90 ikiwa mistari asilima 47 imekwisha jengwa ambapo ni Km 393 toka Tabora.
Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la umeme nchini TANESCO Mhandisi Atanasi Nangali akitoa taarifa alisema mradi wa ujenzi wa kituo hicho unatekelezwa kwa fedha za ndani na nguvu za nishati ya umeme zinatoka Mkoani Shinyanga ukiwa na nguvu ya KV 132 kuja Tabora mjini,Lusu wilayani Nzega.
Mhandisi Nangali amesema serikali imetenga sh.bilioni 4 walipa fidia wananchi 903 na kwamba hadi sasa wamelipa sh.milioni 944 na sh.bilioni 3 zinaendelea kulipwa ambapo mradi huo ulianza rasmi Septemba 18 mwaka 2021 na unatarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka huu 2024.
“Mradi huu unatekelezwa ujenzi wake na kampuni ya kichina TBEA na hadi sasa ujenzi wa umeme toka Tabora hadi hapa umefikia asilimia 10 na hapa kituo cha kupokea,kupoozea na kusafirishia ujenzi umefikia asilima 80,mradi unasuasua kutokana na kasi ndogo ya ulipaji fidia,tutaongeza kasi ili kuruhusu mambo mengine yaendelee kwa wakati”amesema.
Naye Mhandisi Sosipeter Mlalo wa shirika hilo akitoa maelezo kwa Naibu waziri Mkuu kuhusu ujenzi wa kituo hicho alisema kitapokea KV 132 na kitakuwa na transfoma yenye uwezo wa MW 35 ambapo kwa sasa wilaya hiyo inatumia MW 7 .
Mhandisi Mlalo alisema na kwamba kutakuwa na njia 3 za kuja Urambo,3 za kwenda wialayani Kaliua ambapo katika kituo cha Urambo- Ipole wilayani Sikonge ujenzi umefikia asilimia 88 ambapo Mkandarasi kutoka china TBEA anaendelea kufanya kazi nzuri.
Mbunge wa jimbo la Urambo Magreth Sitta amesema kuwa changamoto zinazowakabili wakazi wake ni umeme,maji na mbolea na kwamba serikali inaendelea kuhakiisha inawaondolea hadha hizo kupitia ujenzi wa miradi ya kituo hicho cha umeme,mradi wa maji wa ziwa Victoria na kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo kwa gharama nafuu.
Mbunge huyo amemshukuru marehemu mzee Musa Ludete ambaye alikuwa Diwani wa Kata hiyo ulipo mradi kwa miaka 15 ambapo alijitolea eneo lake lenye hekari 16 kujenga mradi huo ambao unatekeleza kwa nguvu za umma ambapo hadi sasa Zimetumika sh.biloni 16 kujenga n ash.bilioni 24 kuleta umeme.
Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi MNEC kutoka Mkoa wa Tabora Mohamed Nassoro maarufu kama ‘MEDDY’ amesema ujenzi wa vituo hivyo vya umeme Mkoani humo utaleta tija kwa jamii na kufanya changamoto walizokuwa wakizipata kubakia kuwa historia.
Meddy ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi NBS mjini hapa amefafanua kuwa hata tatizo la maji linalowakabili wakazi litakwisha baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi katika wilaya za Urambo, Kaliua na Sikonge ambao utagharimu sh.bilioni 145 kwa kuungannsha maji toka ziwa Victoria Jijini Mwanza.
Amessema kuwa maji kutoka ziwa hilo yanakaribia kufika wilyani Urambo na zimetengwa sh.bilioni 5.9 kutekeleza ujenzi mradi wa maji wa bwawa la Kalemela ambapo alisihi wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali katika kutekeleza miradi yote na watambue kazi inaendelea.
Comments
Post a Comment