VIJIJI 14 ,SIMANJIRO,KITETO KUNUFAIKA NA MRADI MPYA TOKA UCRT
Na Mary Margwe,DmNewsOnline
SIMANJIRO
JUMLA ya Vijiji 14 , kati ya hivyo Vijiji 9 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro na Vijiji 5 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto vinatarajia kunufaika na mradi mpya kutoka Shirika la UCRT Mkoani Manyara, Hali itakayosaidia kuondokana na Migogoro mingi ya ardhi.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la UJamaa Community Resource Team ( UCRT ) Edward Loure wakati wa kuutambulisha Mradi mpya wa " Uhifadhi Jumuishi wa Mazingira na kuboresha maisha ya Jamii katika Halmashauri hizo mbili za Mkoa wa Manyara.
Mradi huo umezinduliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Suleiman Serera katika Mji Mdogo wa Orkesument mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh.Baraka Kanunga, Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Christopher Ole Sendeka, pamoja na madiwani, Maafisa Tarafa, watendaji wa Kata na Vijiji pamoja, viongozi wengine pamoja nawataalam kutoka idara mbalimbali.
Aidha Loure amesema Shirika la UCRT linashughulikia masuala ya kusaidia jamii kusimamia Mipango ya matumizi bora ya ardhi na Utekelezaji sahihi wa Sheria, na hatimaye kuwezesha jamii za asili kumiliki, kusimamia ardhi na kunufaika nayo Kwa lengo la kuboresha maisha yao.
" Lengo kuu la Mradi huu ni kuweka ulinzi wa miliki zaza jamii, kujengea uwezo Taasisi za Vijiji, ili kuweza Kusimamia, kutumia na kunufaika na rasilimali Maliasili katika misingi endelevu " amesema Loure.
" Mimi niende moja kwa Moja kuwapongeza ndugu zetu wa UCRT chini ya Mratibu wake Edward Loure kwa kazi kubwa na nzuri, ambayo mnaifanya na mnaendelea nayo kuzifanya, katika Wilaya yetu ya Simanjiro na Kiteto , kwasababu tunaona matokeo yake mazuri na makubwa yamechangia hata kuondoa baadhi ya Migogoro mkubwa ya ardhi tuliyokuwa nayo katika Wilaya hizi " ndivyo anavyoanza kuzungumza Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dkt.Suleiman Serera.
Dkt. Serera amesema miaka ya nyuma walikua wakiju ukiitaja Wilaya ya Kiteto, Simanjiro kwa mambo ya Migogoro ya ardhi nanhata watu kuzuriana ilikua kazi kubwa sana , lakini UCRT imeganya kazi kubwa na bidii mlioionyesha Kwa kupima kupata matumizi bora ya ardhi mmefanya namna njia inavyoenda na hatimaye mmepunguza kwa kiasi kikubwa sana Migogoro ya ardhi.
" Mimi nikuhakikishie tu Kwa naiba ya Serikali nitaendelea kushirikiana na UCRT ambayo mnakwenda moja kwa moja kwa jamii na kuhakikisha mnatatua changamoto ambazo wananchi wanahitaji, ndugu zangu nataka kusema hakuna jambo gumu duniani kama kumshawishi mzungu Kwa lugha yake akupatie pesa, yaani hilo ni gumu sana, ndio maana UCRT leo tunaipongeza Kwa juhudi zao na kuwa miongoni mwa wanaopata fedha hizo hii ni kwasababu wanajua kuandika proposal ( andiko ) vizuri sana" amesema Dkt. Serera.
Naye Mbunge wa Jimbo hilo Christopher Ole Sendeka amempongeza Mratibu wa mradi huo Edward Loure kwa mambo makubwa ya msingi ya maana sana, awali zaidi ya Vijiji 30 vimeingia katika matumizi bora ya ardhi na Sasa Vijiji 9 pia vimo, hilo ni jambo kubwa sana kwa Maendeleo endelevu ya Wana Simanjiro.
" Mradi huu unakwenda kutoa elimu kwa wananchi, unatoka elimu ya Sera, sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia masuala ya ardhi na wakati mwingine biblia inasema ukishaijua kweli na hiyo kweli itakuweka kuwa huru, nina maana wakati mwingine wananchi wetu wakishajua sera ya nchi inasema Nini katika masuala ya ardhi , Mazito, mifugo basi watakua wapole tu maana tayari wameshaelimishwa na shirika la UCRT, hivyo hongera sana mdogo wangu Edward Loure.
Hata hivyo Sendeka amefafanua kuwa kazi ya kupima vijiji ni kazi ya Serikali nisipokua Serikali kwa sasa haina fedha , waliweza kuwezesha ni mashirika yasiyo ya Kiserikali " Sisia tumshukuri Mungu tu kwamba tumempata mmoja wetu yaani mdogo wangu Edward Loure anaweza kuandikana wazungu wakamkubali, Sasa kazi yetu kubwa ni kumpa tu ushirikiano ili aweze kutimiza ndogo zake " anasema Mh.Sendeka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mh.Baraka Kanunga anasema palipo na Migogoro kamwe Maendeleo huwa ni vigumu kupatikana hivyo kuwepo Kwa UCRT Wilayani Simanjiro ni jambo kubwa linalotakiwa kuungwa mkono wazi wazi.
" UCRT imefanya kazi kubwa sana katika Halmashauri yetu, hivyo ninachowaomba Waheshimiwa Madiwani mpo hapa nawaona, watumishi mbalimbali pia nawaona mpo hakikisheni mnatoa ushirikiano pale mara unapohitajika, msije mkawa ni tatizo huko la kukwamisha kutaendelea Kwa Mipango hii iliyopangwa hapa" amesisitiza Kanunga
Mratibu wa mradi wa UCRT Edward Loure anasema Mchakato wa uibuaji wa mradi huo mpya ulitokana baada ya UCRT kupokea maombi kutoka Halmashauri za wilaya kadhaa zikiwemo hizi za Simanjiro and Kiteto kuomba kufanyiwa michakato ya Mpango ya matumizi ya ardhi.
Mratibu Loure amesema GEF ilipokea maombi Zaidi ya 400 ambapo kati ya hayo, miradi kutoka nchi 9 ziliidhinishwa ukiwemo mradi huu, tuliomba mradi wenye thamani ya dola laki nane na elfu arobaini/USD 840,000, baadaye kiwango hiki kiliongezeka hadi kufikia dola zaidi ya milioni moja na laki nne, ambapo kati ya fedha hizo Wialaya mbiliza Simanjiro na Kiteto tutapata zaidi ya milioni mia nne (400) za Kitanzania, ambapo Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu (2024-2027)
" Vijiji vilivyolengwa na mradi mpya Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mradi imelenga Vijiji vya Ruvuremit, Lerumo, Ngage, Lobosoit B, Gunge, Lemkuna, Lengasiti,Losoito na Naisinyai huku Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto mradi umelenga vijiji vya Makame, Ngabolo, Irkiushioibor, katikati na Ndedo" amesema Mratibu Loure
Comments
Post a Comment