OLE-SENDEKA AFYATULIWA RISASI NNE NA WATU WASIOJULIKANA
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline.
Mbunge wa Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole-Sendeka amefyatuliwa risasi zisizopungua nne na Watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake safarini pamoja na Dereva wake majira ya saa moja leo usiku na kisha watu hao kukimbia muda mfupi baada ya Mbunge huyo kuanza kupiga risasi juu kuwatishia.
" “Ni kweli nimeshambuliwa kwa risasi majira ya saa moja kasoro katika Wilaya ya Kiteto kati ya Kijiji cha Ngabolo na Ndedo, kulikuwa na gari ambayo ilikuwa inanifuatilia kwa nyuma tukawapisha kidogo kama tunataka kuwapisha wapite kulia walipofika usawa wetu wakaanza kumimina risasi kwa Dereva "
Comments
Post a Comment