WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BIDHAA ZA BATTERIES ZINAZOZALISHWA NCHINI.

Timothy Marko DmNews Online 
           
                  DAR ES SALAAM. 

KATIKA kuhakikisha  Sekta ya Uwekezaji inakua kupia Sekta ya Viwanda,  Kampuni ya Izzo  Batteries imekuja kuwekeza Sekta ya Batteries za Magari na Mashine ilikuweza kuhakikisha Watanzania  wananufaika na Bidhaa zinazozalishwa hapa Nchini.

Akizungumza Leo Mei,12 ,2026 Jijini Dar es Salaam  Meneja wa IZO Batteries  IZZO  Mahange amesema kuwa Bidhaa za Batteries  zinazozalishwa kwenye Kampuni hiyo zina dhamana ya miaka 10 ,Ambapo tayari Kampuni hiyo ina mawakala Takribani 150 Nchi nzima. 

"Batteries zetu zinazozalishwa hapa nchini,tayari Kampuni yetu imezalisha Ajira takriban 50" Amesema Meneja Izzo  BATTERIES IZZO Mahange. 

Naye balozi wa Kampuni hiyo Dotto Magari amesema kuwa Bidhaa hiyo ya Bettries Izzo zinaubora kwenye Mashine pamoja Magari, sambamba na Bajaji .

"Hii ni fursa kwa Wawekezaji katika sekta ya Viwanda kuzalisha Bidhaa ya BATTERIES, badala ya kuagiza bidhaa hii kutoka China "Amesema  Balozi wa Izzo Batteries Dotto Magari. 

Magari Ameongeza kuwa lZO  Batteries imekuja nasuluhisho kuokoa Vyombo vya Moto  Nchini Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.