WAJASIRIAMALI WADOGO STENDI YA MAGUFULI WAPATIWA VIZIMBA

  Na Mwandishi wetu DmNewsOnline

            DAR ES SALAAM 


WAJASIRIAMALI wadogo wa Kituo cha Mabasi Stendi ya Magufuli Jijini Dar es Salaam wamekubali kurejea kwenye vizimba walivyopangiwa na uongozi wa stendi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 7,2026 Jijini hapo,John Shayo mmoja wa wafanyabiashara waliorejea kwenye vizimba  kwa niaba ya wenzake amesema kwamba wamekubali  maelekeo waliopewa na uongozi wa stendi hiyo

"Sisi kama wafanyabiashara wadogo tuliokuwa tumeweka biashara zetu ndani ya stendi tumekubali maelekezo yaliyotolewa na uongozi kwamba turudi kwenye vizimba kisha huku tuje kwa ajili ya kufanya biashara za kubeba mikononi tu ",amesema

Naye Mwenyekiti wa Jengo la Abiria,  Haruna Silanda amesema kurejea kwa wafanyabiashara wadogo kumeleta usawa na mivutano isiyo na tija ,hivyo analishukuru kundi hilo kukubali maelekezo yaliyotolewa na uongozi wa stendi na wameonyesha umoja na mshikamano umerejea.

"Kwetu kama viongozi tumepata faraja kuona wenzetu kukubali kurejea kwenye vizimba na hii itasaidia wao kulipa kodi itakayosaidia kuongeza mapato ya stend,i" amesema

Kwa upande wa mjumbe wa jengo la abiria, Rebeca Bigawa ameiomba serikali kurudisha mabasi ya abiria yanayoanzia sehemu nyingine yarudi stendi kuu ya mabasi ili abiria waweze kuongezeka na wafanyabiashara hao waweze kupata wateja kama ilivyokuwa hapo awali.

"Kwa kweli biashara kwa sasa ni ngumu kutokana na baadhi ya mabasi kuanzia safari  zao nje ya stendi kuu na kupelekea kukosekana kwa abiria wengi ndani ya stendi, Ombi letu tunamuomba  Rais wetu atuangalie kwa jicho la huruma ili mabasi yote yaanzia safari zake hapa",amesema

Awali ,Meneja wa Kituo hicho cha stendi ,Isaac Kasebo amesema waliweka utaratibu  ambao walikuwa wakiusimamia , kupanga wafanyabiashara kukaa kwa utaratibu katika maeneo ya kituo yanayotambulika kisheria.

Alisema katika kutekeleza mpango huo walianza na wafanyabishara ambao walikuwa wanapanga biashara zao katika eneo la kushusha na kupakia abiria ambapo kimsingi walijuwa wanafanya makosa.

Aliongeza kuwa kabla ya kuwaondoa walitoa elimu kufuatia na tangazo muda na sehemu wanayotakiwa kwenda kupata vibanda vyao.

Meneja amesema zoezi lakuwaondoa wajasiliamali hao wadogo ndani ya stendi limefanyika juzi Mei 5, 2026  kuwapeleka sehemu husika kwa kuwapatia vizimba vyao  na jambo hilo limekamilika kwa asilimia 100.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.