SUBIRA MGALU :KAMATI TUMERIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA KAMPUNI HII YA ORYX ENERGIES,

 Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

             DAR ES SALAAM 

MWENYEKITI wa kamati ya  Bunge Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo mkoani Pwani mh. Subira Mgalu amesema Serikali inatambua  mchango wa Sekta binafsi Nchini na ndio maana unaweka Mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao,huku wakiridhishwa na uwekezaji wa oryx Energies hapa Nchini.

Mgalu ameyasema hayo  Mei 9, 2026 Jijini Dar es salaam baada ya kamati yake kufanya ziara ya kutembelea Kampuni ya Oryx Energies  ambapo wabunge wamepata nafasi ya kuona namna shughuli za uzalishaji bidhaa mbalimbali za Kampuni hiyo zinavyofanyika ikiwepo vilainishi na gesi ya kupikia majumbani.

Mgalu amesema kamati inatambua mchango na uwekezaji uliofanywa na oryx energy na  katika kipindi Cha miaka minne imeweza kuchangia Pato la Taifa la shilingi Tilioni 1.2 na pia imetoa ajira za moja kwa moja  1000  na kwa  asilimia zaidi ya 90 ni vijana wa kitanzania.

Pia Mgalu  ameongeza kuwa Kampuni hiyo imeweza kutoa ajira zingine kwa  watanzania 25 ambao wanafanya kazi za kusambaza na kuuza bidhaa ( Dillas) za Kampuni ya oryx Energies ambapo uwepo wa Kampuni kwa miaka 25 imekuwa na mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi.

"wabunge wamepata fursa ya kuona mambo mazuri kupitia Kampuni hii ikiwepo maabara ya kisasa inayotumika kupima vilainishi lakini pia kutokana na ajenda ya matumizi ya gesi ya majumbani hivi sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la watumiaji kutoka asilimia  sita ya awali hadi kufikia asilimia 26 kwa wanaotumia gesi hayo ni mafanikio makubwa sana "amesema mh.Mgalu

Amefanunua kuwa kamati yake inaendelea kusisitiza uwekezaji wenye tija na unaoleta matokeo katika taifa letu lakini kubwa mchango wa kuinua uchumi wa nchi na watanzania kwa ujumla wake.

"Tunawapongeza sana kwa maono yenu na tunaishukuru Kampuni hii ya oryx energy kwa kuendelea kutoa mafuta kwani nchi bado Iko salama kwenye mafuta na Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika Sekta binafsi ." amesisitiza  Mgalu 

Ameongeza  katika matumizi ya nishati safi wanampongeza sana mh.rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa kinara wa kuhamasisha na hivi sasa ameweza kutambulika rasmi.katika medani za kimafaifa kwa kazi kubwa anayoifanya na kuwa kinara wa kutunza Mazingira kwa kutumia nishati safi  ya kupikia.

Mh. Mgalu kwa kuhitimisha hotuba yake amesema kuwa kutokana na mambo mengi ambayo wamejionea na kujifunza wao kama kamati wanakwenda kuwa mabalozi wazuri wa oryx energy na changamoto ambazo wameelezwa wamezichukuwa na kwenda kuishauri Serikali kuona namna ya kuzishughulikia.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa oryx Energies Iman Mtafya amesema kuwa kiwanda hicho kilinunuliwa mwaka 1999 ambapo hadi sasa  kinamiaka 25 na uwepo wa kiwanda hicho mbali na mambo mengi lakini kinasaidia kutoa ajira, kukuza uchumi.na kinachangia sh bilioni  300 kwa mwaka sawa na asilimia 0.1.   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.