RC MAKONGORO AIBUKA MSHINDI KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA NCHINi CANADA
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Rukwa ,Charles Makongoro Nyerere ametangazwa kuwa mshindi kupitia droo ya FIFA WORLD CUP 26 ,Fainali ndo Mpango naTemboCardVisa inayochezeshwa na Benki ya CRDB
Katika droo hiyo wamepatikana washindi watatu waliojinyakulia TV Janja Smart za nchi 85 pamoja na king'amuzi.
Washindi hao waliojinyakulia Tv Janja ni Amina Kaswale Awadhi, Esther Dauson Kabakama na Lusekelo Michael Mwamwala.
Makongoro ameibuka mshindi katika droo hiyo pamoja na wenzake wawili kwenda nchini Canada kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia.
Akizungumza kwa njia ya simu na watangazaji wa droo hiyo Charles Makongoro Nyerere amewapongeza kwa kutoa huduma Bora kwa wateja wao na kuelezea furaha yake kwa kuwa miongoni mwa washindi waliopata fursa yakushuhudia Fainali ya Kombe la Dunia.
Naye Meneja Mwandimizi Kitengo cha Kadi CRDB Benki,Karington Chahe amesema washindi wote watasafarishwa ya kwenda na kurudi na benki hiyo na wale waliojinyakulia Tv Janja zitasafirisha kwa gharama za benki hiyo

Comments
Post a Comment