MAFINGA YAENDELEA KUNG’ARA UKUSAJI WA MAPATO YA VUKA LENGO KWA ASILIMIA 105

 Na Mwandishi wetu,DmNewsonline

                      IRINGA 

HALMASHAURI  ya Mji Mafinga imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kufikia asilimia 105 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Mafanikio hayo yameelezwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za robo ya tatu, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Reginant Kivinge, amesema hatua hiyo imetokana na ushirikiano mzuri kati ya madiwani, wakuu wa idara pamoja na watendaji wa halmashauri waliotekeleza majukumu yao kwa weledi na uwajibikaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Fidelica Myovella, amesema halmashauri itaendelea kuzingatia maelekezo ya Serikali ikiwemo kujibu hoja za ukaguzi na kusimamia vizuri ufungaji wa hesabu ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Naye Afisa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Sifael Kivamba, ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato na kuwataka viongozi pamoja na watendaji kuendelea kuongeza juhudi katika mwaka ujao wa fedha.

Katika kipindi hicho, Halmashauri ya Mji Mafinga imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 8.8 dhidi ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 7.5, hatua iliyowezesha kufikia na kuvuka lengo kwa asilimia 105.   


Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.