JESHI LA POLISI YA WASHIKILIA WATU 6 KWA TUHUMA KUKUTWA NA KICHWA CHA MTU

  Timothy Marko DmNewsOnline 

         DAR ES SALAAM. 

JESHI  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamshikilia Said Ali (31) Mganga wa kienyeji nawengine( 5) kwa kukutwa na kichwa chamtu kinachodaiwa James Temba Mkaazi wa kitunda Wilaya ilala. 

Akizungumza Leo May 13,2026 jijini Dar es Salaam Kamishina wa Kanda Maalumu CP.Murilo Jumanne Murilo amesema kuwa mnamo March 30 Mwaka huu jeshi hilo lilianza Uchunguzi wa Shauri hilo nakuwabaini watu sita ambao majina yao yamehifadhiwa kwa Uchunguzi zaidi akiwemo Mganga huyo kudaiwa kuhusika na tukio hilo. 

"Tunawashikilia watu sita ikiwemo Mganga Said Ali maarufu SIDE kwakuhusika na shauri hilo,taratibu za kisheria zinaendelea kuhusiana na shauri hili" Amesema Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu CP.Murilo Jumanne Murilo. 

CP Murilo Ameongeza kuwa Nivyema Wananchi wakawa watulivu juu ya ufuatiliaji wa kichunguzi  kwa kushirikiana jeshi hilo na taasisi zingine zakiuchunguzi.

"Tukio hili nibaya kwa Binadamu linapaswa kulaniwa,katika Uchunguzi wetu Mtumishiwa huyo alituonesha sehemu yamtuhumiwa huyo mahali palipofukiwa mwili wa James Rojers Temba" Alisisitiza  Kamishina Murillo Jumanne Murilo.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.