DC MSANDO ATOA MAAGIZO KWA TANESCO NA TARURA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

    Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

              DAR ES SALAAM 

JESHI la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam limeungana na wazimamoto duniani kuadhimisha Siku hiyo katika maonesho yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam 

Akizungumza katika Maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Wakili Albert Msando ametoa maagizo kwa Jeshi la  Zimamoto na Uokoaji kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) pamoja na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) kuwa ujenzi wa  miundombinu ya Barabara na wale wanaounganisha umeme kuwa makini ili inapotokea majanga  ya moto iwe rahisi kuyadhibiti.

Amesema  Zimamoto wanatakiwa kujiridhisha ubora wa vifaa vinavyotumika kuunganisha umeme kwenye  maeneo ya biashara,masoko na maduka wahakikishe vifaa hivyo viko salama,kama haviko salama aliyeunganisha huduma hiyo achukuliwe hatua za kisheria.

Kwa upande wake  Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoti na Uokoaji Tanzania na Msemaji wa Jeshi hilo DCP Puyo Nzalayaimisi aimeishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kulipatia vifaa vya kisasa na magari ambayo yatarahisisha utendaji wa kazi ya uokoaji yanapotokea majanga.

"Jeshi hilo litaendelea kujitoa kwa hali na Mali na kwa moyo wa dhati kwa ajili yakuwahudumia wananchi",amesema   

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.