DIWANI MALILO ATOA MSAADA KWA WATOTO WASIOJIWEZA SHULE YA MSINGI BONYOKWA
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline Dar es Salaam DIWANI wa Kata ya Bonyokwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mhe.Tumike Malilo ametoa msaada wa sare za shule ,kalamu na daftari kwa watoto wasiojiweza katika shule ya msingi Bonyokwa Akizungumza na waandishi wa habari Leo Januari 29,2026 mara baada ya kukabidhi msaada huo amesema kwamba ameamua kutoa msaada kwa watoto hao kuonyesha upendo na kujitoa kwa ajili ya jamii inayomzunguka katika Kata hiyo. "Nimeona ni vema kuwasaidia watoto wasiojiweza kwa kuwapatia msaada wa sare za shule ili nao watambue kuwa tunawapenda na kuwathamini",amesema Mh.Tumike Aidha,amesema tunaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya,elimu na miundombinu ya Barabara. Sekta ya Elimu Akizungumzia sekta ya elimu Diwani huyo amesema kwamba katika Kata ya Bonyokwa Ina shule Mbili za msi...