WAUMINI KATOLIKI WAZIDI KUWAPINGA KITIMA, RUWA'ICHI ,WASEMA HOJA ZA SIASA ZACHOCHEA MGOGORO
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM UPINZANI wa waumini wa Kanisa Katoliki dhidi ya mwenendo wa baadhi ya viongozi wa juu wa kanisa, akiwemo Padri Dkt. Charles Kitima na Askofu Mkuu Ruwa’ichi, unaendelea kushika kasi, huku hoja za kimaadili, kisheria na kiteolojia zikiwekwa wazi hadharani. Kupitia tafakuri nzito ya dhamiri iliyotolewa na Mwalimu Ludovick Joseph, muumini wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, waumini wameanza kujenga hoja ya pamoja kwamba Kanisa si mtu mmoja, si padri wala askofu, bali ni jumuiya ya waumini, na kwamba viongozi wa kanisa hawako juu ya Injili wala juu ya waumini. Katika tafakuri hiyo, waumini wanasema wazi kuwa kuhoji, kukosoa na kuomba uchunguzi dhidi ya kiongozi wa kanisa si uasi, si dhambi wala si chuki, bali ni haki ya kisheria inayotambuliwa ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki lenyewe. “Kanisa ni takatifu kwa sababu ya Kristo, lakini viongozi wake ni wanadamu wenye mipaka na wanaweza kuk...