DK.MWINYI:CCM ITAFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KWA SERA ZENYE TIJA KWA WANANCHI

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline ZANZIBAR RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kuahidi kuwa CCM itafanya kampeni za kistaarabu zitakazozingatia Utamaduni, Silka na Desturi za Wazanzibari. Dkt. Mwinyi amechukua fomu hiyo katika Afisi za Tume ya Uchaguzi leo, tarehe 30 Agosti 2025, asubuhi, na hatimaye msafara wake ukaelekea Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kupitia Barabara ya Miembeni, Kariakoo, Rahaleo na Michenzani, akisindikizwa na mamia ya wanachama wa chama hicho waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabara. Aidha, Dkt. Mwinyi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, na kisha kuzungumza na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi afisini hapo. Akizungumza na mamia ya wanachama wa CCM katika Uwanj...