AMEIR MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CHAMA CHA MAKINI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI SEPT,2

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

          DAR ES SALAAM 

CHAMA cha Makini kinapenda kuwataarifu wananchi na wanachama wake,vyombo vya habari kuwa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 zitafanyika  katika Viwanja vya Bakhresa Manzese Jijini Dar es Salaam Septemba 2,2025 kuanzia saa nane kamili mchana na mgeni rasmi katika uzinduzi ni Ameir Hassani Ameir Mgombea Urais wa Serikali ya Mapunduzi Zanzibar kupitia Chama cha Makini

Katika uzinduzi huo,Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Coaster Kibonde pamoja na mgombea Mwenza,Azza Haji Suleiman wanatarajiwa kuhutubia wananchi na kueleza kwa kina sera na vipaumbele vya Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Makini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.

Aidhaa ,viongozi wakuu wa chama,wagombea ubunge ,na wagombea wa udiwani kutoka mikoa mbalimbali nchini watashiriki katika tukio hilo kubwa la kihistoria na la kisiasa.

Wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya Jirani  mnakaribishwa kuhudhuria kwa wingi katika uzinduzi huo wa kampeni ili kupata nafasi na fursa ya kusikiliza sera zinazolenga kuleta maendeleo ya nchi na kwa ustawi wa Mtanzania

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.