Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, Dkt. Michael Chabai. Na Yusuph Mussa,DmNewsonline KILINDI MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Dkt. Michael Chabai amesema barabara za wilaya hiyo bado ni changamoto, na kueleza moja ya sababu ya wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya chini ni kutokana na changamoto ya barabara hizo. Ameyasema hayo Agosti 22, 2026 wakati anafungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, na kuongeza kuwa jitihada zinahitajika kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanafanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara za vijijini ili kuona wakulima wanakuwa na uwezo wa kwenda kuuza mazao yao sokoni. "Barabara zetu kwenye wilaya yetu bado ni changamoto, na hii inasababisha mazao ya wakukima wetu kuuzwa kwa bei ya chini. Hivyo tunataka kuona barabara hizo zinapitika ili wakulima wetu waweze kufikisha mazao yao sokoni" alisema Dkt. Chab...
Comments
Post a Comment