MDAU WA MAENDELEO IRINGA MJINI NDUGU SUFIAN MGUDE AKABIDHI KITUO CHA POLISI ,RC JAMES ATIA NENO.
Na Eliasa Ally DmnewsOline
IRINGA
JUMLA ya shilingi milioni 58 zimetumika katika ujenzi wa kituo Cha Polisi kilichojengwa katika Kata ya Mseke Tanangozi wilaya ya iringa mjini chini ya ufadhili wa mdau wa maendeleo Sufian Mgude .
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho kilichojengwa na mdau wa maendeleo wilayani humo Sufian Mgude ,mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James amempongeza mdau huyo nakusema kwamba amefanya jambo jema kwa kukumbuka alikotoka.
Amesema kuwa uwepo wa kituo hicho karibu utasaidia kupunguza viendo vya uhalifu kwani awali ilikuwa wanafuata huduma mbali na eneo hilo hivyo jambo kubwa kwa wananchi ni kushirikiana na Jeshi la Polisi na pia kuacha kujichukulia sheria mkononi.
"Nakupongeza sana ndugu Mgude kwani ulichofanya ni kitu kikubwa na wachache sana wanakumbuka walikotoka lakini wewe licha ya kuishi nje ya mkoa wa Iringa lakini bado umekumbuka kuunga mkono Serikali katika kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma "amesema mkuu wa mkoa James
Kwa upande wake mdau huyo amesema amejenga kituo hicho cha Polisi kwa lengo la kuendeleza ushirikiano na taasisi za Serikali na kufikisha huduma kwa jamii hasa katika masuala ya usalama na kupunguza uhalifu.
Amesema kuwa wakati wa mchakato huo kulikuwa na vipingamizi mbalimbali hasa kupata eneo la ujenzi ambapo baadhi ya wananchi walionyesha kupinga kwa kuwatisha wauzaji wa eneo hadi pale ambapo mkuu wa mkoa kipindi yuko mkuu wa wilaya alipoingilia kati na kuanza ujenzi ambao umezinduliwa rasmi.
Amesema kuwa gharama halisi zilizotumika hapo ni sh. milioni 58.1 ambapo pia eneo ambapo kituo kimejengwa lilinunuliwa kwa shilingi milioni 15 ili litumike na jeshi hilo na kumpongeza mwananchi aliyekubali kuuza eneo hilo la jirani.
Amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho ni kuongeza usalama ili jamii iendelee kuwa salama katika maendeleo ya uchumi wa taifa na ujenzi huo pia unalenga kuwa mwarobaini kwa wakazi wote wa Kata ya ya Mseke pamoja na maeneo jirani ya kata hiyo kuondokana na gharama za nauli kufuata huduma eneo la Ifunda au Iringa mjini. 

Comments
Post a Comment