ACT WAZALENDO WAKIMBILIA MAHAKAMANI KUPINGA MAAMUZI YA INEC
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnlie
DAR ES SALAAM
CHAMA Cha ACT Wazalendo kimeamua kukimbilia Mahakamani kwenda kupinga maamuzi ya Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) kutokana na kumuondoa mgombea wao wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Luhaga Mpina ambaye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilibaini mapungufu ya kisheria na kikanuni kuhusiana na uyeuzi wake,mapungufu yanayompotezea sifa za kuwa mgombea halali wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Agosti 27,2025 Jijini Dar es Salaam,Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Omar Said amesema kwamba ACT Wazendo haikubaliani na maamuzi hayo kutokan na kile walichodai kuwa yamefanywa kinyume na Sheria na Katiba.
"Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) haina mamlaka kisheria kumiengua mgombea yoyote wa nafasi yoyote kwa kufuata maelekezi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ama taasisi youote ,badala yake mtu au taasisi inaruhusiwa kuweka mapingamizi kwa mgombea inayemtilia shaka,"amesema Mwanasheria Mkuu ACT Wazalendo Omar Said
Aidha,amesema kwamba nakala ya Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyotumwa Tume Huru ya UchaguI haijaonesha sehemu yoyote ambayo Msajili wa Vyama vya Siasa inaiomba Tume Huru ya Uchaguzi kumtengua mgombea wao,hivyo kuendelea kuhoji uharaka wa INEC kuchukua maamuzi.
"Tumeamua kukimbilia Mahakamani kwa sababu Mahakama ndio chombo cha mwisho chakutoa haki hapa mchini,hivyo ni imani Yao hoja zao zitapokelewa ma kukubalika",amesema Mwanasheria Mkuu ACT Wazalendo Omar Said 



Comments
Post a Comment