SEKTA YA KILIMO YAINUA MAISHA YA WAKAZI KASULU
Na Allan Kitwe,DmNewsonline KASULU HALMASHAURI ya Mji Kasulu ni miongoni mwa halmashauri 8 za Mkoa wa Kigoma ambapo asilimia 80 ya wakazi wake wanaishi Vijijini na shughuli kuu ya kiuchumi katika maeneo hayo ni kilimo. Maboresho makubwa ya sekta ya kilimo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan yameleta tija kubwa kwa wakazi wa halmashauri hiyo na Wilaya nzima ya Kasulu. Akiongea na gazeti hili hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Vumilia Simbeye ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia, halmashauri hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia sekta hiyo. Amebainisha mambo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita ambayo yamechochea mafanikio makubwa kwa wakazi wa halmashauri hiyo kuwa ni kuongezwa bajeti, ugawaji mbolea ya ruzuku na kutafuta masoko ya kutosha. Haya yamepelekea wakazi wengi wa halmashauri hiyo kuchangamkia sekta ya kilimo hali a...