SIMBA YAINGIA MKATABA MNONO WA SHILINGI BILIONI 20 NA BETWAY
Timothy Marko DmNewsonline
DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba Sports Club Nchini Tanzania imeingia mkataba wa Shilingi bilioni 20 wa miaka mitatu na Kampuni ya Ubashiri ya michezo hususani Mpira wa miguu ya Betway.
Akizungumza naWaandishi wa Habari Jijini katika Hafla ya makabidhiano ya Hundi ya Mkataba huo Mjumbe wa bodi ya wa kurugenzi Klabu ya Simba Salimu Abdallah Muhene Try Again amesema Makubaliano hayo ya udhamini kati ya Betway na Klabu ya Simba unalenga kukuza jina la timu hiyo kitaifa na Kimataifa.
"Kampuni yoyote inapenda kushirikiana na Kampuni yenye hadhi Kimataifa yenye nguvu,Sisi kama Simba tutahakikisha tunailinda Brand hii ya Betway" Amesema Try again.
Try again Ameongeza kuwa Katika Mkataba huo kutakuwa na Uwazi ili kuhakikisha pande zote mbili zina nufaika na Mkataba huo.
Amesisitiza kuwa nivyema wapenzi na Mashabiki wa timu ya Simba kuhakikisha wanakuwa wa moja ili kuweza kuiletea Maendeleo Klabu hiyo.
"Kuanzia Sasa wapenzi wetu wa Klabu ya Simba tuwape sapoti Betway ili mdhamini huyu apate anacho kitaka"Try again.
Kwaupande wake Mdhamini Mkuu wa Kampuni ya Ubashiri wa Mpira ya Kimataifa Betway Africa Jason Shield amesema kuwa Kampuni hiyo imeenea Nchi nyingi Duniani ambapo Kampuni hiyo inajiendesha kwa mifumo ikiwemo Matumizi ya Application ambayo nirafiki zaidi kwa Wateja.
Amesema kuwa Wateja watakao bashiri kutumia Kampuni hiyo ya Betway watapata Huduma Bora.
" Lengo letu nikuweza kukuza Sekta ya Michezo kwakushirikiana na Wateja na Mashabiki wa Klabu ya Simba Sports Club" Amesema Mdhamini Mkuu wa Betway Jason Shield.
Aidha kwaupande wake Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani amesema kuwa Makubaliano hayo ya udhamini kati Klabu ya Simba Sports Club na Kampuni ya Kubashiri Michezo ya Betway yanatokana na ligi kuu ya Tanzania kuwa ya nne kwa U Bora Barani Afrika.
Amesema kuwa Nivyema Vilabu vya Mpira vikawa wazi na Kampuni hiyo ya Betway ilikuepukana Sura Mbaya kwenye tasnia ya Soka.
"Tusitumie muda mwingi kusema tunapata Hasara,Bali Vilabu vitumie Mudamwingi katika kuwekeza" Alisema Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Tanzania Athuman Nyamlani. 


Comments
Post a Comment