ULYANKULU WAPONGEZA KASI YA RAIS SAMIA KUBORESHA ELIMU
![Image](https://lh3.googleusercontent.com/-bURuuxewBMY/Z5zQBCe-SOI/AAAAAAAAN2g/88YqutZ4mxEgVLlGtVKiB-Sdw4NAoPAIACNcBGAsYHQ/s1600/IMG_ORG_1738329818583.jpeg)
Na Allan Kitwe,DmNewsonline KALIUA WAKAZI wa Tarafa ya Ulyankulu, Jimbo la Ulyankulu, Wilayani Kaliua Mkoani Tabora wamepongeza juhudi kubwa zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya 6 kwa kuboresha miundombinu ya elimu katika vijiji na kata zote. Wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa Tarafa hiyo ni miongoni mwa tarafa zilizokuwa na shule chache na miundombinu hafifu lakini kasi ya serikali ya awamu ya 6 imeleta neema kubwa Jimboni humo. Mkazi wa Kata ya Ichemba Annaemmy Mazigo ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Mkindo amempongeza Rais wa awamu ya 6 Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipa sekta ya elimu kipaumbele kikubwa na kutenga bajeti ya kutosha. Ameeleza kuwa katika shule ya Mkindo sekondari amepeleka zaidi ya sh mil 500 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 4 na matundu 10 ya vyoo ili kuboresha miundombinu ya sh...