SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa mwaka 2024 wameweza kutoa dawa za kingatiba za kudhibiti na kutokomeza magonjwa mbalimbali.
Magonjwa hayo kama Watu 257,358 kati ya 265,217 walipatiwa kingatiba za kutokomeza ugonjwa wa matende na mabusha kutoka kwenye Halmashauri za Mtama na Mtwara Mikindani (sawa na asilimia 97),.
Watu 5,462,851 kati ya 6,447,157 kutoka katika Halmashauri ishirini na nne (24) walipatiwa kingatiba ya ugonjwa wa Usubi (sawa na asilimia 85), watu 1,603,425 kati ya 1,967,143 kutoka Halmashauri saba (7)
Halmashauri hizo ni Ngorongoro DC Monduli DC, Longido DC, Kiteto DC, Simanjiro DC, Mpwapwa DC na Kalambo DC, walipatiwa kingatiba za ugonjwa wa trakoma sawa na asilimia 82. Watoto wenye umri wa kwenda shule (yaani umri wa miaka 5-14) 9,896.694 walilengwa kupatiwa huduma ya kingatiba kwa ugonjwa wa minyoo ya tumbo ambapo hadi kufikia Disemba 2024 watoto 8,676,234 sawa na asilimia 88 walimeza kingatiba hiyo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 30,2025 katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam siku ya kilele Cha maadhimisho ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Duniani.
Serikali kwa kushirikiana na wadau hutoa huduma kwa wananchi ambao tayari wamepata athari za magonjwa hayo ikiwemo upasuaji kwa watu wenye tatizo la ugonjwa wa mabusha ambapo kwa mwaka 2024 watu 1,084 wamepatiwa huduma ya upasuaji na wagonjwa 2,412 wenye tatizo la vikope wamerekebishwa kope bila malipo.
"Kaulimbiu ya mwaka huu ni Tuungane, Tuchukue hatua, Tutokomeze Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele"
Kwa upande wa ugonjwa wa usubi, Mpango umepata mafanikio ya kudhibiti ugonjwa huo kama tatizo la kiafya la kijamii kwa kupunguza maambukizi kwa binadamu kutoka wastani wa asilimia 45% kabla udhibiti hadi wastani wa asilimia 5% baada ya udhibiti katika Halmashauri 30 hapa nchini. Kwa upande wa magonjwa ya minyoo ya tumbo na kichocho ambayo ni tatizo kwenye jamii katika Halmashauri zote 184, juhudi za kuyadhibiti zinaendelea na takwimu za wagonjwa wanaoripotiwa zinaashiria kuwa maambukizi katika ngazi ya jamii yamepungua sana.
Hata hivyo amesema njia za kutokomeza magonjwa hayo ni pamoja na kushiriki katika kampeni za kumeza kingatiba kila mwaka na kufuata kanuni za Afya ikiwa ni kuzingatia usafi wa mazingira, usafi binafsi, kubadili tabia hatarishi, kunawa mikono kila wakati na kutumia vyoo bora
Comments
Post a Comment