RC CHALAMILA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA TRC KUONA NAMNA YA KUJENGA RELI NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kwamba uongozi wa mkoa utakutana na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kufanya mazungumzo ya kuangalia uwezekano wa kujenga reli yakusafirisha abiria ndani ya mkoa ili kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Jiji hilo na kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa saa 24.
Hayo yamebainishwa leo Januari 30,2025 wakati wa kutoa mrejesho wa mkutano wa Nishati Afrika uliofanyika kwa siku mbili Januari 27 na 28,2025 hapa Nchini ambapo lengo la mazungumzo na shirika la reli ni kuangalia namna ya kujenga reli kwa fedha za ndani zinazokusanywa na Halmashauri ili kupunguza adha ya usafiri.
Aidha,amesema ujenzi wa reli hiyo na njia ambayo itajengwa utajulikana baada ya watalaam kufanya upembuzi yakinifu na kuona sehemu gani inapaswa kujengwa.hivyo Wataalumu watakuja na majibu.
Mbali na hilo Chalamila pia ametangaza kuanza kwa utaratibu wa wafanyabiashara katika Jiji la Dar es salaam kufanya shughuli zao kwa masaa 24 kuanzia Februari 22 mwaka huu.
“Katika kuelekea kufungua zaidi mkoa wa Dar es Salaam mimi na wenzangu tumekubaliana Dar es Salaam ianze kufanya biashara saa 24,kwa maana hiyo Februari 22 ndio itakuwa siku rasmi yakufungua nakwamba awali walipanga kuaza Februari nane.
“Awali tulipanga Februari 8,2025 lakini tumepeleka mpaka Februari 22 kwa sababu kuna baadhi ya maeneo hatujafikia kuyaweka taa na maboresho mengine madogo madogo,”amesema Chalamila.
Mbali na hilo ofisi ya mkuu wa mkoa wamekubaliana mambo mbalimbali kutokana na mji huo kukua kwa kasi ikiwemo masuala ya kuboresha majengo chakavu.
“Kutokana na mji wetu kukua kwa kasi tumekubaliana yafuatayo kuunda kamati maalum kuangalia majengo chakavu na yaliyochoka,baada ya hapo kamati itashirikiana na wenye majengo kutafuta wafadhili ili kuyaboresha majengo hayo yaendane na taswira ya Jiji la Dar es salaam”amesema Chalamila.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wafanyabiashara katika soko la Ushirika Kariakoo Hawa Ghasia amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa kwa ajili ya kuboresha soko dogo la kariakoo ambalo limegharimu kiasi cha bilioni 28.03 na mpaka sasa marekebisho hayo yamefikia asilimia 97 na wanatarajia kuanzia kesho Januri 31,kupandisha majina ya wafanyabiashara waliokuwepo awali kabla ya soko hilo halijaungua.
“Kesho tunaanza zoezi la kupandisha majina ya wafanyabiashara wa awali,nitoe rai ambao wanadaiwa walipe madeni yao ili kupunguza usumbufu wakati wa kugawa vizimba lakini wale ambao ni wafanyabiashara wapya wanapaswa kutulia na wasidanganyike kama kuna mtu kati watamlipa ili wapate nafasi watakula hasara .
Amesema nafasi zote zitaombwa kwa kutumia mfumo wa TAUSI na hivi karibuni tutakutana nao na tutawaelekeza jinsi ya kutumia mfumo huo kuomba nafasi”,amesema Ghasia.
Comments
Post a Comment