RC CHALAMILA :DAR ES SALAAM KUANZA BIASHARA MASAA 24 IFIKAPO FEBRUARI 22,MWAKA HUU.
Na Angelina Mganga ,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema wageni wote waliokuja katika mkutano wa Nishati ambao uliofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam imeisha salama na wageni wote wameondoka salama.
Amesema mikutano kama hii imezoeleka kufanyika katika nchi zingine duniani lakini kwa awamu hii Tanzania imeandaa mkutano huo kutoka katika mataifa mbalimbali ya Afrika.
RC Chalamila ameyasema hayo leo Januari 30 ,2025 mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam amesema mkutano huo umeleta tija kubwa kwa Mkoa wetu kwa Yale yote ambayo yamefanikiwa ni wazi kwamba Kuna mafanikio makubwa hususani.katika eneo la miundombinu ya umeme
Pia amesema Jiji la Dar es salaam litaanza kufanya shughuli za biashara kwa masaa 24 ambapo uzinduzi utafanyika Februari 22,2025 wafanyabiashara wataanza rasmi.
Aidha ,amesema zoezi hilo limechelewakuwa kwasababu baadhi ya maeneo kama uwekaji wa taa pamoja na kamera bado havijakamilika lakini hadi kufikia tarehe hiyo shughuli zote zitakamilika na biashara zitaanza rasmi.
Akizungumzia kuhusu soko la Kariakoo amesema kuwa ujenzi wake umefikia asilimia 97 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kutoa bilioni 26 kulipa kwa wakandarasi kwa ajili ya kuhakikisha soko hilo linafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kufikia viwango vya Kimataifa pamoja na kurudisha wafanyabiashara wapya.
Kuhusu majengo kutokana na ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam .amesema wanakwenda kuunda kamati ambayo itakagua majengo itaangalia namna ya kuweza Kufanya ujenzi mbalimbali hasa majengo ya kibiashara na nyumba za kulala wageni ,kumbi zaikutano lakini pia wataendelea kuweka Mazingira wezeshi ya usafi ili kuhakikisha jiji linakuwa safi.
Pia amesema kupitia Halmashauri zote za jiji la Dar es salaam wanajipanga kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kwani ni aibu jiji la Dar es salaam kupata magonjwa ambayo yanatokana na uchafu hivyo tutaandaa sheria na kanuni zitakazosimamia usafi kwa Jiji pamoja na kuweka vyombo vya kuweka takataka maeneo yote.
Hata hivyo amesema wanakwenda kukutana na mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogoso ili kuona namna ya kuongeza reli za abiria kutokana na msongamano kwenye eneo la usafiri huku akiwataka waandishi wa habari kuendelea kufanya kazi ya kutoa taarifa kwa wananchi hasa taarifa sahihi ambazo zinatakiwa kwenda kwa wananchi .
Kwa upande wake wa Mwenyekiti wa Soko la Ushirika Kariakoo Hawa Ghasia amesema wafanyabiashara watatumia mfumo wa Tausi Kuomba ili kupata eneo la kufanyika biashara.
Comments
Post a Comment