WAZIRI WA ELIMU PROF.MKENDA:SERA YA ELIMU SASA KUZINDULIWA FEBRUARI 1,2025.
Na Deborah Lemmubi.DmNewsonline
DODOMA
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolph Mkenda mapema Leo hii ametangaza mabadiliko madogo kwenye tukio la Uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 uliotakiwa kufanyika kesho tarehe 31 Januari 2025 na utafanyika tarehe 1 Februari 2025 kutokana na dharula ambayo imeshindwa kuzuilika na kufanya ratiba hiyo kusogezwa kidogo.
Waziri ameyasema leo Januari 30,2025 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko yaliyojitokeza katika kuelekea Uzinduzi huo.
Na kuongeza kuwa pamoja mabadiliko hayo ya tarehe mpya 1 Februari lakini Mgeni rasmi bado atabaki kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Leo nimewaita hapa kueleza mabadiliko kidogo kwenye tukio la Uzinduzi wa Sera ya Elimu ambalo lilikuwa lifanyike kesho Januari 31 2025,lakini kwasababu ya dharula ambayo imeshindwa kuzuilika tukio hilo sasa lonasogezwa mbele mpaka tarehe 01 Februari 2025 na Mgeni rasmi bado ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengi wa Kitaifa watashiriki".
Aidha Waziri ametumia wasaa huu kuwaomba radhi na uvumilivu wale wote ambao wamekwisha kuanza safari kwa usumbufu utakao jitokeza na wale ambao bado hawajaanza safari amewaomba kusogeza mbele ili kuendana na tarehe hii mpya.
"Suala liliotokea ni la dharula kwaweli halikuweza kuzuilika,tunajua wapo watu wengi wameanza safari za kuja tunaomba watuvumilie na wabaki hapa Dodoma na wale ambao hawajaanza safari wanaweza kusogeza mbele kidogo ili waendane na tarehe mpya".
Na kusisiatiza kuwa hili ni suala kubwa na la Kitaifa linalogusa kizazi hiki nq vijavyo mbele ya safari.
Comments
Post a Comment