Posts

Showing posts from January, 2024

SERIKALI YATOA BILIONI 24 KUBORESHA UWANJA WA NDEGE TABORA

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline  TABORA  SERIKALI ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha sh bil 24.6 kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji uwanja wa ndege Tabora ambapo jengo jipya la abiria la ghorofa mbili limeanza kujengwa. Akizungumza baada ya kutembelea uwanja huo juzi, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amemshukuru Rais Samia kwa kuwapatia kiasi hicho cha fedha ili kuufanyia maboresho makubwa uwanja huo. Amebainisha kuwa mradi huo ambao umeanza kutekelezwa mwaka jana unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hivyo kuwezesha ndege nyingi na kubwa kutua katika uwanja huo na kupatikana huduma muhimu zote. ‘Mkandarasi alitakiwa kumaliza kazi hii mwezi Machi 2024 lakini ameomba kuongezewa muda zaidi kutokana na vifaa vilivyoagizwa kutoka nchini India na China kuchelewa kufika’, alisema. Profesa Mbarawa amemwagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi huo Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Company Ltd kuhakikisha ...

MADIWANI KIBAHA WAJADILI KUUNDWA KWA MAMLAKA YA MAJI ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIYO.

Image
Na Mwandishi Wetu DmNewsOnline  KIBAHA BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha limeshauri kuundwa mamlaka ya maji ili iweze kuhudumia wananchi wa Mji huo Kwa lengo la kukabiliana na changamoto za upungufu wa maji safi. Hayo yamesemwa leo Januari 31 2024 na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mussa Ndomba wakati wa kikao cha Madiwani kilichofanyika Mjini Kibaha. Ndomba amesema kuwa inashangaza kuona maji yanayokwenda Jijini Dar es Salaam yanapitia Kibaha lakini eneo hilo wananchi wanakabiliwa na changamoto kubwa ya maji. "Tunafikiri imefika wakati sasa Kibaha nayo kuwa na Mamlaka yake badala ya kutegemea nyingine ambayo inahudumia Dar es Salaam kwa asilimia kubwa,"amesema Ndomba. Ameongeza kuwa Kibaha ikiwa na Mamlaka yake itakuwa ni rahisi kukabili changamoto kwani itakuwa na mipango na bajeti yake tofauti na ilivyo sasa haipewi kipaumbele kutokana na kutokuwa na Mamlaka yake.

WAZIRI MAKAMBA ANADI FURSA ZA BIASHARA, UWEKEZAJI ITALIA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline ITALIA WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  January Makamba (Mb.) amenadi fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini katika mkutano wa wafanyabiashara, viongozi wa siasa na wa kijamii nchini Italia. Katika mkutano huo, Waziri Makamba amewaeleza wafanyabiashara na wawekezaji wa Italia fursa mbalimbali za biashara zinazopatikana nchini  pamoja na mageuzi makubwa ya kuboresha mazingira ya uwekezaji yanayofanyika chini ya Uongozi imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri Makamba amesema mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni salama na rafiki kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha wafanyabiashara wanatekeleza majukumu yao katika mazingira rafiki na salama.  Kadhalika Waziri Makamba amesema kuwa Tanzania inazingatia misingi ya utawala bora pamoja na kuzungukwa na nchi saba ambazo hazina bandari na hivyo kurahisisha usafirishaji wa bidhaa...

GST YATOA ELIMU YA JIOLOJIA YA MIAMBA NA MADINI KWA WANAFUNZI

Image
 Na Mwandishi Wetu DmNewsOnline  DAR ES SALAAM ZAIDI ya wanafunzi 20 w,a darasa la tatu kutoka shule ya msingi Reader Rabbit, Bay bridge iliyopo jijini Dar es Salaam wamefika Makumbusho ya Taifa ya Jiolojia Tanzania ili kujifunza Jiolojia ya Miamba na Madini yapatikanayo Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mafunzo hayo yametokewa leo Januari 31, 2024 na Wataalamu wa Makumbusho hayo kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) baada ya wanafunzi hao kutembea Makumbusho hayo. Akizunguza katika ziara hiyo, Mwalimu wa shule hiyo ambaye pia ni kiongozi wa timu hiyo Ringo Iringo amefurahishwa na aina za miamba na madini yaliyomo kwenye Makumbusho hayo ambapo amesema wanafunzi wake wamejifunza mengi kuhusina na Jiolojia ya Miamba na Madini yapatikanayo Tanzania na Afrika kwa ujumla. Sambamba na hayo Iringo amesema wanafunzi wake wamejifunza Jiolojia ya Tanzania, Afrika na ulimwengu mzima kwa nadhalia hivyo uongozi wa shule hiyo ukaona umuhimu wa kufika katika Makumbusho ...

NEEC YATOA USHAURI MZITO KWA WANAWAKE NA VIJANA

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), BengI Issa, amewataka wanawake na vijana kutumia vizuri na kwa nidhamu fedha inayotolewa na taasisi za uwezeshaji, ili kasi ya kujikwamua kiuchumi iongezeke na fedha inayopokelewa iwe na matokeo chanya. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake  na Vijana wa Kanisa la TAG City Light Temple, Goba, jijini  Dar es Salaam, Issa amesema serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan ina nia nzuri na wazi ya kuwawezesha Watanzania kiuchumi kwa kutoa mitaji wezeshi, hasa kwa makundi maalumu kwa kutumia majukwa ya uwezeshaji.  Amesema kasi ya kujikwamua kiuchumi itaongezeka na kuwa na matokeo chanya iwapo wawezeshwaji watatumia vizuri na kwa nidhamu fedha na raslimali zingine wanazopewa kupitia majukwaa hayo kwenye  maeneo yao. "Ni matumaini yangu wanawake na vijana wa Goba mtalitumia vizuri jukwaa hili kujiimarisha kiuchumi kwa kupata mikopo...

TANZANIA YASISITIZA MPANGO WA MATTEI UZINGATIE MAHITAJI STAHIKI YA AFRIKA

Image
 Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline    WAZIRI  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia amesisitiza umuhimu wa mpango wa Mattei kuzingatia mahitaji sahihi ya Afrika ili uweze kuleta matokeo stahiki barani Afrika. Makamba amesema kuwa mpango huo ukizingatia mahitaji stahiki ya Afrika changamoto nyingi zinazokabili nchi zilizoendelea zinazosababishwa na ukosefu wa maendeleo barani Afrika zitaondoka. Awali akihutubia katika mkutano wa Nne wa Italia-Afrika, Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni amesema mpango wa Mattei utagusa masuala ya usalama wa nishati na matumizi ya nishati mbadala, maendeleo ya miundombinu, usalama wa chakula, elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na kupambana na wahamiaji haramu, ameeleza  Serikali ya Italia inatarajia kushiriki kwa kiasi kikubwa kukuza maendeleo ba...

DC SAME AWATAKA WANANCHI KUITUMIA VIZURI WIKI YA SHERIA ILI KUPATA UELEWA MPANA.

Image
 Na Mwandishi Wetu DmNewsOnline SAME MKUU  wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewaongoza wakazi wa wilaya hiyo katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria wilayani humo na kusisitiza usimamizi wa sheria katika kulinda mazingira hasa maeneo yaliyo hifadhiwa. Amesema wilaya ya Same ni kati ya maeneo yaliyo athiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu na kusababisha kukosa Mvua kwa miaka mitatu mfululizo, hata hivyo Mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu zimeleta madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa miundombinu, Mazao mashambani na baadhi ya makazi ya watu kuharibiwa. Kaslida ameyasema hayo wilayani humo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo yanafikia kilele januari 30 mwaka huu . “Pamoja na shughuli yenyewe kutoa elimu ya sheria, mmefanya jambo moja la msingi sana ambalo sasa ni kaulimbiu yetu wilaya ya Same ya kuhakikisha tunapanda miti na kuifanya wilaya inakua ya kijani naomba mtumie sheria mnazo zisimamia kuhakikisha miti inalindwa”.amesema  N...

RAIS SAMIA APELEKA BIL 5 KUCHIMBA BWAWA KUBWA LA MAJI URAMBO

Image
Na Allan Vicent, DmNewsOnline TABORA WAKAZI wa Vijiji vya Kalemela A na B katika kata ya Muungano Wilayani Urambo Mkoani Tabora wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea kiasi cha sh bil 5.9 kwa ajili ya kutekelezwa mradi mkubwa wa Bwawa la Maji utakaowezesha wananchi kupata maji safi na salama ya kunywa. Wakizungumza na gazeti hili juzi wamesema kuwa ujio wa mradi huo ni mkombozi kwao kwa kuwa utamaliza kilio chao cha miaka mingi cha ukosefu wa huduma ya  maji safi na salama katika vijiji vyote vya kata hiyo na maeneo mengine. Zebedayo Lukungu (50) mkulima, mkazi wa Kijiji cha Kalemela A ameeleza kuwa ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa vijiji hivyo ulipelekea wengi wao kuugua magonjwa ya kuhara mara kwa mara na ndoa nyingi kuvunjika. ‘Tunamshukuru sana mama yetu Rais Samia kwa kutuletea mradi huu, sasa tuna uhakika wa kunywa maji safi na salama ya bomba mwaka huu, tunachoomba mafundi waongeze bidii ili ukamilike kwa wakati’, amesema. Mfanyabiashara Hussei...

MANISPAA TABORA WAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADAWATI 9,500

Image
Na Allan Vicent, DmNewsOnline TABORA HALMASHAULI ya Manispaa Tabora inakabiliwa na upungufu wa madawati 9,500 katika shule za msingi na sekondari ili kuwezesha kila mtoto kukaa kwenye dawati pindi wawapo darasani. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Luis Bura alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya miundombinu ya shule za msingi na sekondari katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika hivi karibuni  katika ukumbi wa halmashauri hiyo. Amesema kuwa upungufu huo unapaswa kutatuliwa haraka iwezekanavyo ili kwenda na kasi ya maboresho makubwa ya miundombinu ya shule zote yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya 6 ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. DC Bura amesisitiza kuwa ili kufanikisha upatikanaji madawati hayo wananchi, wadau na taasisi mbalimbali wanapaswa kushirikishwa ili watoto wote wanaoripoti shuleni wapate sehemu ya kukaa. ‘Tunahitaji michango ya hali na mali katika kipindi hiki, naomba taasisi zote zilizopo hapa manispaa zikiwemo asasi za kira...

WAZIRI WA KAIRUKI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA TANAPA, ALITAKA KUJA NA UBUNIFU WA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline  ARUSHA  WAZIRI wa  Maliasili  na Utalii, Angellah Kairuki  ametoa maelekezo mazito  kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kulitaka  libadilike ili liweze  kuchangia ipasavyo kwenye  uchumi wa taifa  kupitia utalii na kuhifadhi rasirimali  kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye. Kairuki ametoa maelekezo hayo leo Januari 29,2024 kwenye hafla ya uvalishaji cheo na uapisho wa Kamishna  wa uhifadhi,Musa Kuji katika. Kwenye ofisi za  Makao  makuu ya TANAPA jijini Arusha. Amesema kuwa  katika kipindi hiki Shirika la  TANAPA  linatakiwa kuja na  ubunifu wa hali ya  juu katika kutangaza vivutio vya utalii  na  kubaini mazao mapya  ya utalii ili sekta ya utalii iweze  kufikia lengo la Ilani  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya  kuwa  na wageni  milioni tano na kuliingizia taifa jumla ya dola  za kimarekani bilioni sita ifika...

WIZARA YA MADINI, TANESCO, FARU GRAPHITE WAJADILI CHANGAMOTO YA UMEME MRADI WA MAHENGE

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline   UJUMBE  wa Wizara ya Madini ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo, umekutana na Uongozi wa Kampuni ya Faru Graphite inayotekeleza Mradi wa Mahenge Graphite pamoja na na Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) kwa lengo la kujadili changamoto ya nishati ya umeme inayokabili Mradi wa Mgodi wa Madini ya Kinywe Mahenge. Kwa upande wa Kampuni ya Faru Graphite, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Black Rock Mining na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Faru Graphite John de Vries, umewasilisha hoja kadhaa wakati wa kikao ikiwemo changamoto ya nishati ya umeme na miundombinu ya barabara ambako pande zote zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kutoa huduma hizo. Wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika Leo Januari 29, 2024 katika ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma ni pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Black Rock Mining, Paul Sims, na Msha...

UTOAJI HATI WASITISHWA_ ARUSHA

Image
    Na Mwandishi Wetu DmNewsOnline ARUSHA KAMISHNA wa Ardhi Mkoa Arusha, Geofrey Msomsojo amezuia zoezi la utoaji hati za umiliki wa ardhi, katika eneo la ekari sita, lililopo kata ya Olmoti katika jiji hilo kutokana na eneo hilo kuwa na mgogoro kwa miaka 17 sasa, ikiwa ni utekelezaji agizo la siku 30 la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaa. Waziri Slaa wiki iliyopita, alitembelea eneo hilo na kuzungumza na  William Mollel ambaye analalamika eneo lake kuvamiwa pamoja na majirani wa eneo. Katika mgogoro huo, familia ya Mollel inamtuhumu aliyekuwa Ofisa Ardhi jiji la Arusha, Chritopher Kitundu ambaye hivi sasa amehamishiwa wilaya ya Tandahimba kuuziwa eneo na Leah Neeva hilo kinyume cha sheria. Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kitundu alikana kuvamia eneo hilo na kueleza wanaomlalamikia waende mahakamani badala ya kumtuhumu kuvamia eneo lao. “Mimi sijavamia eneo la mtu, kama kuna wanaonilalamikia basi waende mahakamani, ndipo haki inaweza kupatik...

KIBAHA YAPOKEA GARI LA WAGONJWA ,MBUNGE ATIA NENO

Image
Na Mwandishi wetu DmNewsOnline  KIBAHA HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha imepokea gari ya wagonjwa ambayo itatumika katika Hospitali ya Wilaya hiyo na kuondoa kero iliyokuwepo awali iliyosababishwa na uhaba wa magari hayo. Kwasasa Halmashauri hiyo Ina magari manne ya wagonjwa huku kikwazo kikielezwa kwamba kiliikuwepo zaidi katika kituo cha afya Mlandizi ambacho kipo Mjini. Akikabidhi gari hilo  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo alitoa tahadhari katika matumizi ya gari hilo kutumika kama daladala ya kubebea watendaji. Mwakamo alisema Ili gari hilo lidumu kwa muda mrefu linatakiwa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa  lisiharibike mapema. "Gari hili linakuja kuondoa kikwazo Cha uhaba wa magari kilichokuqepo awali, natoa angalizo lisitumike kama daladala ya kubebea watendaji wanapoenda kazini, pandeni daladala, bajaji sio kupanda kwenye hili gari mkifanya hivyo tatizo litarudi tena," alisisitiza. Mwakamo alijivunia jitihada z...