DC SAME AWATAKA WANANCHI KUITUMIA VIZURI WIKI YA SHERIA ILI KUPATA UELEWA MPANA.
Na Mwandishi Wetu DmNewsOnline
SAME
MKUU wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewaongoza wakazi wa wilaya hiyo katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria wilayani humo na kusisitiza usimamizi wa sheria katika kulinda mazingira hasa maeneo yaliyo hifadhiwa.
Amesema wilaya ya Same ni kati ya maeneo yaliyo athiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu na kusababisha kukosa Mvua kwa miaka mitatu mfululizo, hata hivyo Mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu zimeleta madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa miundombinu, Mazao mashambani na baadhi ya makazi ya watu kuharibiwa.
Kaslida ameyasema hayo wilayani humo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo yanafikia kilele januari 30 mwaka huu .
“Pamoja na shughuli yenyewe kutoa elimu ya sheria, mmefanya jambo moja la msingi sana ambalo sasa ni kaulimbiu yetu wilaya ya Same ya kuhakikisha tunapanda miti na kuifanya wilaya inakua ya kijani naomba mtumie sheria mnazo zisimamia kuhakikisha miti inalindwa”.amesema
Nakuongeza kuwa "Kesi Zinapokuja kwenu zinazohusiana na masuala ya uharibifu wa mazingira naomba mzitilie mkazo sana kwa sababu wilaya yetu imepitia kipindi kigumu cha kukosa mvua miaka mitatu mfululizo na ndio maana tumeamua kuwekea kipaumbele uala hili la kupanda miti na kuitunza”.Alisema mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni.
Pia Kaslida amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutumia kipindi chote cha maadhimisho hayo kupata elimu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria kwakua asilimia kubwa ya watu wamekua wakikosa haki zao kwa kutojua sheria, suala ambalo serikali imeona kuja na utaratibu wa kuadhimishwa wiki ya sheri kujenga ukaribu baina ya wataalam na jamii.
Awali Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Same Mhe.Chrisanta Chitanda amesema maadhimisho hayo yalianza mapema tangu Januari 24 kwa kutoa elimu kupitia mabanda ya maonesho,mikutano mbalimbali na kutembelea maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo Shuleni, shughuli ambazo ni endelevu hadi siku ya kilele februari Mosi mwaka huu 2024.
Comments
Post a Comment