MADIWANI KIBAHA WAJADILI KUUNDWA KWA MAMLAKA YA MAJI ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIYO.


Na Mwandishi Wetu DmNewsOnline 
KIBAHA

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha limeshauri kuundwa mamlaka ya maji ili iweze kuhudumia wananchi wa Mji huo Kwa lengo la kukabiliana na changamoto za upungufu wa maji safi.

Hayo yamesemwa leo Januari 31 2024 na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mussa Ndomba wakati wa kikao cha Madiwani kilichofanyika Mjini Kibaha.


Ndomba amesema kuwa inashangaza kuona maji yanayokwenda Jijini Dar es Salaam yanapitia Kibaha lakini eneo hilo wananchi wanakabiliwa na changamoto kubwa ya maji.

"Tunafikiri imefika wakati sasa Kibaha nayo kuwa na Mamlaka yake badala ya kutegemea nyingine ambayo inahudumia Dar es Salaam kwa asilimia kubwa,"amesema Ndomba.

Ameongeza kuwa Kibaha ikiwa na Mamlaka yake itakuwa ni rahisi kukabili changamoto kwani itakuwa na mipango na bajeti yake tofauti na ilivyo sasa haipewi kipaumbele kutokana na kutokuwa na Mamlaka yake.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025