KIBAHA YAPOKEA GARI LA WAGONJWA ,MBUNGE ATIA NENO
Na Mwandishi wetu DmNewsOnline
KIBAHA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha imepokea gari ya wagonjwa ambayo itatumika katika Hospitali ya Wilaya hiyo na kuondoa kero iliyokuwepo awali iliyosababishwa na uhaba wa magari hayo.
Kwasasa Halmashauri hiyo Ina magari manne ya wagonjwa huku kikwazo kikielezwa kwamba kiliikuwepo zaidi katika kituo cha afya Mlandizi ambacho kipo Mjini.
Akikabidhi gari hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo alitoa tahadhari katika matumizi ya gari hilo kutumika kama daladala ya kubebea watendaji.
Mwakamo alisema Ili gari hilo lidumu kwa muda mrefu linatakiwa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa lisiharibike mapema.
"Gari hili linakuja kuondoa kikwazo Cha uhaba wa magari kilichokuqepo awali, natoa angalizo lisitumike kama daladala ya kubebea watendaji wanapoenda kazini, pandeni daladala, bajaji sio kupanda kwenye hili gari mkifanya hivyo tatizo litarudi tena," alisisitiza.
Mwakamo alijivunia jitihada zake za kuleta maendeleo katika Jimbo hilo huku akiishukuru Serikali kwa namna inavyotoa fedha na vitendea kazi kumaliza kero za Wananchi.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dk.Wilford Kondo alieza kwamba hakuna mgonjwa atakayetizwa fedha kwa huduma ya gari hilo la wagonjwa na kwamba atakayedaiwa fedha ya mafuta atoe taarifa.
Kadhalika Dk Kondo aliwataka Wananchi kufika kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya kwani huduma nyingi kwasasa zinapatikana katika Hospitali hiyo tofauti na awali ambapo ilikuwa lazima mgonjwa apewe rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Diwani wa Mlandizi Euphrasia Kadala akiishukuru Serikali kwa kutoa gari hilo la wagonjwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ambalo sasa litakwenda kuondoa adha ya kukodi magari pindi lililopo linapopata hitilafu.
Tatu Haji na John Pilly ni wakazi wa Mlandizi ambao wanaishukuru Serikali kwa ajili ya gari hilo litakalosaidia kuhudumia wagonjwa kwa haraka.
Comments
Post a Comment