NAIBU WAZIRI NDERIANANGA ASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MHE. JAJI MWANAISHA KWARIKO
![Image](https://lh3.googleusercontent.com/-GqPmkqwbwN0/Z3L9zkWWisI/AAAAAAAAMVI/SVqG5N9WWIUM3eEweAp0YHvPm-fNAoEbQCNcBGAsYHQ/s1600/IMG_ORG_1735589176928.jpeg)
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameshiriki dua maalum ya kumuombea marehemu Mheshimiwa Mwanaisha Athumani Kwariko, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC) Tarehe 29 Disemba, 2024 nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam. Dua hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Profesa Ibrahim Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. James Henry Kilabuko, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe. Jaji George Kazi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania akiwemo, Mhe. Asina Omari na Mhe. Balozi Omary Mapuri. Akitoa salamu wakati wa dua hiyo Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Profesa Ibrahim Juma ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliofikwa na msiba huo hu...