ANJITA YAVIWEZESHA VIKUNDI VYA KILIMO CHA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA PEMBEJEO ZA MILIONI SHILINGI MILIONI 10.7



Na Mwandishi Wetu, DmNewsOnline.
PWANI 

TAASISI ya Anjita Child Development Foundation ya Kibaha imetoa pembejeo za milioni 10.7 kwa wakulima wa bustani za mbogamboga.

Wakulima hao wa bustani ni vikundi ambavyo vinatoka kwenye Vitongoji vya Mwanabwito na Kidai Kata ya Kikongo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi kuwezesha jamii kupitia kilimo cha bustani na kukabidhi pembejeo  kwa vikundi hivyo Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Evelyn Ngwira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha amevitaka vikundi hivyo kuzingatia ratiba za kilimo.

Ngwira amesema kuwa mradi huo wa uwezeshaji jamii ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha afya na utasimamiwa na wanajamii wenyewe na watapaswa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Anjita Janeth Malela amesema kuwa mradi huo umeibuliwa na wananchi wenyewe na wataundesha kwa kusimamiwa na taasisi na wataalamu wa kilimo.

Malela amesema kuwa pembejeo hizo ni ufadhili kutoka Ubalozi wa Marekani ukiwa na lengo la kuongaza kipato kwa familia na kuboresha afya kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidai Samson Dotto kwa niaba ya diwani wa Kata ya Kikongo amesema kuwa kilimo ni uti wa mgongo kwani wao wanafanya shughuli hizo kando ya Mto Ruvu na utawasaidia kiwasogeza mbele kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Naye ofisa kilimo kata ya Kikongo Fortunatus Ng'itu amesema kuwa hiyo ni fursa muhimu kwa wananchi na wanapaswa kuitumia ili kubadili maisha yao.

Moja ya wanufaika wa mradi huo Eliwaza Kingu amesema kuwa wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia mradi huo kwani utawasaidia kuwapunguzia gharama za kununulia pembejeo ambazo ni kubwa.

Daila Lubawa amesema kuwa kupatiwa pembejeo hizo kutawasaidia kuongeza ukubwa wa maeneo yao ya kilimo ambapo walikuwa wakipata changamoto ya pembejeo ambapo baadhi ya vifaa walikuwa wakiazimana.

Kitongoji cha Mwanabwito ni vikundi  3 ambavyo vina watu 9 na kimoja kina watu 10 kwa Kitongoji cha Kidai kuna vikundi 6 vyenye watu 6 isipokuwa vikundi 2 vina watu 5.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025