WAUMINI WAASWA KUMTEGEMEA MUNGU
Na Angelina Mganga ,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
KASISI wa Mtaa wa Mtakatifu Marko Malamba Mawili Mbezi Dayosisi ya Dar es Salaam Kanisa Anglikana Tanzania Rev.Fr.Kelvin Dismas amewaasa waumini wa Dini ya Kikristo kumtegemea Mungu kwani kuiona Christmas ya mwaka huu ni kwa neema ya Mungu mwenyewe.
Akihubiri katika ibada ya adhimisho la kuzaliwa Yesu Kristo, Padre Dismas amesema kuzaliwa kwake kuna makusudi mengi ikiwemo
kuukomboa Ulimwengu, tena yeye ndiye asili ya
baraka,tumaini na furaha hivyo Yesu Kristo azaliwe ndani ya mioyo yetu ili makusudi ya kuja kwakwe ulimwenguni yatimie kwenye maisha yetu.
"Amezaliwa kwa ajili yetu mwokozi wa ulimwengu,Yesu Kristo alizaliwa ili kuwakomboa wanadamu katika dhambi ,yeye ni mshauri wa ajabu",amesema Kasisi Dismas
Aidha,amewataka waumini kutazama kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika namna ya rohoni zaidi. Kristo azaliwe ndani yetu lakini kuwa na kiasi kwa mambo ya mwilini kwani pasipo na kiasi kunaweza kuleta madhara .
"Tunaposherehekea Christmas hii tumshukuru Mungu kwa mapenzi yake kwetu kwa kutufikisha siku ya leo,kutulinda na kututunza",amesema Kasisi Dismas
Pia amewatakia Mwaka Mpya mwema waumini wote na wasio waumini uwe mwaka wa baraka kujiwekea malengo na kumshirikisha Mungu Kwa mambo yote uwe mwaka wa utulivu na amani.
Kwa upande wake Katibu wa Mtaa Amani Ndahani amemshukuru Mungu kwa kuiona Christmas hii tangu mwaka jana hadi leo mapenzi ya Mungu kutuwezesha na kututunza tunauona mkono wa Mungu Kila iitwapo Leo kwani waumini wanaendelea kuongezeka.
Naye Mwenyekiti wa UMAKI Mtaa Grace Chikoko amesisitiza waumini kupenda kuhudhuria ibada kwani kumcha Mungu ni chanzo cha hekima.
Comments
Post a Comment