DISEMBA 31 TAASISI ZA SERIKALI IWE MWISHO MATUMIZI YA MKAA NA KUNI.
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
TAASISI zote za Serikali zilizopo katika mkoa wa Dar es salaam ambazo zinahudumia watu zaidi ya 100 zimetakiwa kutekeleza bila shuruti agizo la Waziri Kassimu Majaliwa Majaliwa kuwa ifikapo Disemba 31,2024, ziache kutumia Nishati chafu zitokanazo na ukataji wa kuni na mkaa .
Akizungumza leo jijini Dar es salaam,kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albeth Chalamila ,Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Temeke Abdalah Mtinika wakati kuadhimisha kilele cha wiki yakuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia ijulikayo kama rafiki briquettes inayozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Mtinika amesema kuwa kutokana na agizo hilo la Waziri Mkuu ni matumaini yake viongozi wenzake wa mkoa wa Dar es salaam watatekeleza agizo hilo bila shuruti hivyo watafanya ukaguzi kwa kila taasisi ili kuona utekelezaji wa agizo hilo.
" haya tunayoyaona leo ni mapinduzi makubwa katika nishati ambayo yanaenda kuacha alama kubwa kwa vizazi vyetu chini ya mbeba maono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu agenda ya matumizi ya nishati safi na salama ili kuokoa mazingira ambapo amekuwa ni mpambanaji wa kweli kuhakikisha jamii ya watanzania inaondokana na matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa inayotokana na miti ifikapo mwaka 2033"Amesema Mtinika
Amesema kuwa ubora wa nishati hiyo ya rafiki briquettes umethibitishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS),na kufanyiwa utafiti wakutosha tangu mwaka 2018 na taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Taasisi ya Utafiti na Maendeleo (TIRDO) pamoja na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) hivyo niwahimize wananchi kutumia nishati hii ya rafiki briquettes kutokana haina madhara yeyote kiafya.
Aidha amesema kuwa nishati hiyo ya rafiki briquettes inatokana na makaa ya mawe na kuchanganywa na vumbi la sukari guru.
"Makaa ya mawe yanazalishwa kutoka kwenye mgodi wa Kiwira unaomilikiwa na STAMICO uliopo mkoa wa Songwe ambao una hifadhi ya zaidi ya tani milioni 300 ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 100 ijayo hivyo niwatoe hofu wananchi kuwa kuna siku moja kutatokea uhaba wa nishati hii ya rafiki briquettes"Amesema Mtinika
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi imekuwa ni tishio dunia mzima hali ambayo imepelekaifa makubwa kuweka maazimio mbalimbali ikiwemo azimio lakutunza mazingira lakini pia azimio lakuachana na nishati chafu ambayo inaadhili afya za binadamu.
"Kupelekea maadhimio hayo mheshimiwa Rais wetu Dkt samia Suluhu Hassan alitangazwa kama kinara wakuhamasisha matumizi ya nishati safi Afrika na duniani ,sasa sisi kama stamico tulitumia ubunifu tukafanya utafiti wa bidhaa tulizonazo ikiwemo madini tuliyo nayo,rasili mali tulizo nazo ni namna gani na tutumie teknolojia gani sayansi gani ili kubadilisha kwenda kwenye nishati safi yakupikia ambayo hii tuliyoizindua"amesema Mwasse
Comments
Post a Comment