CHALAMILA AWATAKIA WATANZANIA SIKUKUU NJEMA SHEREHEKEENI KWA AMANI NA UTULIVU.



Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila leo Disemba 23,2024 amezungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa muhimu kuhusiana na maendeleo ya mkoa huo kuelekea katika sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya.

Chalamila amewatakia  wakazi wa Dar es Salaam heri ya Christmas na mwaka Mpya na Watanzania wote kwa ujumla washerehekee kwa amani na utulivu.

"Ameipongeza sekta ya habari kwa kazi kubwa na nzuri yakuipigania serikali na kuelimisha umma huku akiwatakia Wakristo na wasio wakristo kusherehekea sikukuu ya Noel kwa amani na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani", amesema

Aidha amesema kwamba vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Jiji.

Pia ametoa ufafanuzi wa matukio matatu yaliyoleta taharuki katika Mkoa wa Dar es Salaam na kupelekea maswali mengi ya sintofahamu ambapo ameyataja matukio hayo ambapo tukio la mtoto aliyepotea,Jeshi la polisi lilifanya kazi kubwa ya kumtafuta na kumpata akiwa ametumbukia ndani ya kisima.

Kabla ya Jeshi la Polisi halikufanikiwa kumuona taarifa zilisambaa mtandaoni ya kuwa mtoto huyo ametekwa.Amefafanua hakutekwa kama ilivyodhaniwa awali Bali ametumbukia kwenye kisima kilicho pembezoni mwa Madrasa.

Katika tukio la pili ni tukio la baba harusi Vincent Masawe aliyejiteka na gari ya kuazima na kwenda kujificha kwa mganga wa kienyeji.

Katika tukio jingine ni tukio la mfanyabiashara Ulomi ambaye alipata ajali akiwa hana kitambulisho hata kimoja,baada ya ajali kutokea alipelekwa hospitali moja kwa moja,Mkuu wa Mkoa alieleza Jeshi la Polisi limefafanua utaratibu kwamba majeruhi wanapaswa kutibiwa bila kuwana fomu ya PF3.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na watanzania wote kwa ujumla kuwa na mazoea yakutembea vitambulisho vyao vya Taifa (NIDA) ili kurahisisha utambuzi unapokutana na changamoto yoyote.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025