MLAWA AWASHIKA MKONO JUMUIYA YA WAZAZI IRINGA MJINI.
Eliasa Ally,DmNewsOline
IRINGA
MDAU wa Maendeleo kutoka Wilaya ya Kilolo Aidan Mlawa amechangia mifuko 50 ya saruji na mashine maalumu ya kuchapisha karatasi 'photocopy machine' kwa Jumuiya ya wazazi Iringa Mjini.
Mlawa ametoa Mchango huo katika balaza la kikanuni la kufunga Mwaka alipohudhuria kama Mgeni Rasmi.
"Nimesikia risala yenu kuwa mnauhitaji wa nyumba ya watumishi naomba nianze kwa kuchangia mifuko 50 ya sumenti ya kuanzia panapokwama tutaendelea kuwasiliana" Amesema
Mbali na hilo Mlawa ameahidi kuchangia mashine maalumu ya kuchapisha karatasi kwa ajili ya matumizi ya JUMUIYA.
Akitoa shukrani Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Masanyika amempongeza mdau huyu kwa moyo wake wa kuchangia chama na shughuri mbalimbali za Maendeleo.
"Naomba nitoe shukrani kwa niaba wa wajumbe wenzangu mchango huu ni Mkubwa sana kwetu kwa makadilio tu ni zaidi ya milioni 2 haya ni mapenzi ya dhati sana tukuahidi tu tuko pamoja na tutaendelea kushirikiana" Alisema Masanyika
Comments
Post a Comment