TMA YATOA TAHADHARI MWENDELEZO WA MVUA ZA VULI NOVEMBA 2024 HADI APRILI ,2024
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg3cQprQuMFF2TktJI263hAMpUTd4w1l8FeCypaJGqWAY7aDID5Y-10pOS-VaeUHg5UMmiAPm2b_zns05w1wKqtz0ctAFjXEFjrsfDKm_VEbnAspf3cu2tyutffN7ZV56NEGz9h6m_fG5Q/s1600/IMG_ORG_1730440541582.jpeg)
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline DAR ES SALAAM MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza muelekeo wa msimu wa mvua za vuli ambazo zimeanza Novemba 2024 na kuishia mwezi Aprili,2025. Akizungumza na Waandishi wa habari Oktoba 31 ,2024,Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Dkt.Ladislaus Chang'a amesema kutokana na mabadiliko ya hali ya mifumo ya hali ya mvua nchini inaonekana kupungua kupelekea mvua katika maneno mengi kuwa chini ya wastani. Taarifa ya tahadhari imetolewa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mifumo mingi inaonyesha joto kuongezeka Duniani ukilinganisha na mwaka 2023, kwenye usawa wa Bahari maeneo mengi ya Kusini mwa Bahari ya Hindi. Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2024 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka kwa Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani ikijumuis...