AIDAN MLAWA AMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA
Na Eliasa Ally,DmNewsOline
IRINGA
MDAU wa Maendeleo wilaya ya kilolo na Mkurugenzi wa kampuni ya john Galt Hauliers LTD Usafirishaji Mizigo Ndani Nje ya Tanzania. Aidan Mlawa ampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa letu la Tanzania
Mlawa ameyasema hayo mapema wiki hii katika mahojiano na DmNewsonline ambapo amesema Rais Dkt.Samia amefanya Maendeleo makubwa ndani ya uongozi wake amepeleka Maji vijijini, umeme standad gej, Elimu bure, tren imerahisisha wafanyabiashara wanaenda Dodoma kwenda kufanyabiashara kwenda na kurudi na huduma hiyo imewarahisishia wananchi wote
Mama Samia amefanya mamiradi makubwa ndani ya nchi hii Ambapo sisi wafanyabiasha tukienda nchi za nje tukisema tunatoka nchinij Tanzania wanatamani kuja Kuwekeza Tanzania viwanda,mashamba na vitu mbalimbali
Mlawa amesema ili Mama Samia aendelee kufanya Mambo makubwa inatakiwa sisi wafanyabiashara na Wananchi inatupasa tulipe Kodi ili Rais tumuunge mkono kuendeleza miradi mikubwa zaidi ya hapa inayoifanya katika Taifa letu
Watanzania inatupasa kujivunia Rais wetu anaewapenda watanzania wote na amewapa Uhuru wafanyabiashara wote wadogo na wakubwa kufanya Biashara zao Kwa Uhuru na kuwasikiriza changamoto zao na kuzitatua
Comments
Post a Comment