KATIBU MKUU CCM DKT NCHIMBI KUWASILI LINDI LEO ,KUHUTUBIA WANANCHI VIWANJA VYA MLIPILI.




Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
LINDI

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), DKt. Emmanuel Nchimbi leo alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Lindi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Mpilipili, Mjini Lindi.

Balozi Nchimbi na msafara wake, atapokelewa rasmi asubuhi ya leo katika Ofisi za CCM za Mkoa huo, ambapo atafanya kikao na Kamati ya siasa na baadaye mkutano wa ndani wa makundi mbalimbali. 

Lengo la ziara hiyo ni  Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba mwaka huu.

Katika ziara hii Dkt Nchimbi kabla ya kuingia mkoani Lindi, amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, ambapo ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025