Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline LINDI ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, inayoendelea katika mikoa ya Kusini, akianzia Mtwara na sasa yuko Lindi, imewahamisha viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema walioamua kujiunga CCM leo, wakisindikizwa na mamia ya wanachama waliorejesha kadi zao za vyama vya zamani kwa kasi kubwa kwenye mkutano wa hadhara. Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mpilipili, Lindi mjini, ukiwa ni mwendelezo wa ziara ya Balozi Nchimbi, amewapokea viongozi hao waandamizi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mchinga Ndugu Hamidu Bobali. Wengine ni viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Wanawake wa ACT Wazalendo Lindi Mjini Bi. Hawa Kipara, Meneja Kampeni wa Wabunge ACT Wazalendo Lindi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF Lindi Issa Sapanga, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mwenyek...