SEKTA BINAFSI YAPEWA KIPAUMBELE KUPITIA TRENI YA SGR
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wizara ya Uchukuzi imetoa Kipaumbele kwa Sekta binafsi katika kushirikiana kwenye uwekezaji wa treni ya kisasa SGR ili kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Shirika la Reli Tanzania ( TRC )kwa kushirikiana na wizara ya uchukuzi linawakaribisha sekta ambazo sio za kiserikali katika kuweza kuongeza chachu ya maendeleo ya Treni ya kisasa ya SGR.
“Tumejenga reli hii kwa kuweza kurahisha biashara mbalimbali nchini kwetu Tanzania kwani ni nchi pekee ambayo tunatumia mtandao mkubwa wa reli ya kisasa yenye kilomita 720 na kupitia reli hii mizigo ndiyo itakayoleta faida kubwa na kukuza pato la taifa huku wasafiri wa kawaida wakiwa na muitikio mkubwa wa kutumia treni hiyo .
Aidha serikali imeweza kutumia Dolla Milioni 3.138 kukamilisha ujenzi wa reli huku Shilingi Trillion 1.3 zimetumika kununua vitendea kazi vikiwemo mabehewa 89, seti 10 za vichwa vya treni ya mchongoko na vichwa 19 vya treni ya umeme”.amesema Profesa Mbarawa.
Tumeona wananchi wengi kutoka maeneo jirani wamefurahishwa na huduma hizo hivyo wanatumia usafiri huo wa treni katika kukuza na kuendeleza uchumi kutoka kwenye serikali yetu.
Hata hivyo Profesa Mbarawa ameongeza kuwa kupitia uzinduzi huo wa treni za kisasa SGR kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma unaenda kufanyika Jijini Dodoma Agosti 1,2024 huku mgeni rasmi wa uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . Samia Suluhu Hassan .
Comments
Post a Comment